Akizungumza mara baada ya upasuaji huo, Dkt. Victor Ngotta, Bingwa wa Upasuaji wa Watoto wa MNH, amesema mafanikio hayo yanaonyesha uwezo wa hospitali kushughulikia kesi ngumu na adimu zinazohitaji utaalamu wa hali ya juu, na ni hatua muhimu katika kuendelea kuimarisha huduma za upasuaji wa kibingwa nchini.
Dkt. Ngotta amesema upasuaji huo ulihitaji maandalizi ya kina na ushirikiano wa wataalamu kutoka fani mbalimbali kutokana na hali ya kipekee ya mtoto huyo, ambaye alikuwa na pacha aliyekuwa na mikono, miguu na sehemu ya kiuno pekee huku akimtegemea mwili wa mwenzake kwa ukuaji na uhai.
Mafanikio ya upasuaji huo yanaendelea kuimarisha nafasi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kama kituo kinachoongoza nchini katika utoaji wa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi.
Mtoto anaendelea vizuri na yupo chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...