Na Victor Masangu,Kibaha

Mwenyekiti wa Jumuiya ya  wanawake (UWT) Wilaya ya  Kibaha mjini Elina Mgonja katika kuunga mkono juhudi  za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuwakomboa kiuchumi ameamua kutoa darasa la mafunzo ya ujasiriamali.

Akizumgumza katika ziara maalumu ambayo ameifanya kwa wanawake wa UWT  katika kata mbili za Kongowe na Kibaha ikiwa  ni  utekelezaji wa ahadi yake ambayo ameitoa  ya kuwapa ujuzi na mafunzo ya kutengeneza bidhaa mbali mbali.

Mgonja amebainisha kwamba ameamua kutoa mafunzo kwa lengo la kuwapatia ujuzi wanawake hao ambao utawasaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kujiajiri na kupambana na wimbi la umasikini.

",Nimeamua kutimiza  kujitolea kuwafundisha Wanawake wa UWT jinsi  ya kutengeneza Sabuni,Vitenge vya Batiki,mafuta ya aina mbalimbali na mambo mengine ya kijasiriamali kwakuwa nataka kuona kila mwanamke anatumia fursa kupitia mafunzo waliyoyapata."amebainisha  Mgonja.

Mgonja amesema kwamba amelenga kufanya ziara hiyo maalumu kwa ajili ya kutoa darasa la ujasiriamali katika kata zote 14 zilizopo ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha.

Mgonja amewaomba Wanawake wa UWT Kibaha Mjini kuhakikisha wanajitokeza kushiriki katika fursa mbalimbali zinazotolewa hususani za kijasiriamali ili waweze kupata elimu  ambayo itawasaidia katika kuondokana na kuwa tegemezi.

"Mimi kama mwenyekiti wenu wa UWT nipo katika ziara yangu kwa ajili ya kufanya mafunzo na darasa maalumu la ujasiriamali na leo tumefanya somo katika kata ya Kongowe na Kata ya Kibaha,"amebainisha Mwenyekiti

Katibu wa UWT Wilaya ya Kibaha Mjini Cesilia Ndaru amewahimiza  Wanawake wa kujitokeza kwa wingi  kushiriki darasa la  mafunzo hayo kwa kuwa yanatolewa bure bila malipo  ya aina  yoyote

Ndaru amesema kipindi hiki ni kipindi cha kufanyakazi na hakuna uchaguzi wowote na kwamba kama kuna mtu anawaza uchaguzi ni wazi kuwa anajipotezea muda ambapo amewaomba Wanawake kuungana na Mwenyekiti katika mafunzo hayo ya ujasiriamali.

Nao baadhi ya wanawake kutoka kata za Kongowe na Kata ya mkuza wamemshukuru Mwenyekiti wa UWT Kibaha mjini kwa kuwawezesha mafunzo hayo ya ujasiriamali ambayo yatawawezesha kujikwamua kiuchumi.

Ziara ya  Mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake ( UWT) Wilaya ya  Kibaha Mjini yenye lengo la kutoa mafunzo ya ujasiriamali  yamefanyika katika kata mbili za Kongowe na Kibaha.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...