Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Ndg. Abdi Mahmoud Abdi, amesema ataendelea na zoezi la kukagua mali za CCM kwa lengo la kuzifahamu kwa undani, kubaini changamoto zinazozikabili na kuweka mikakati ya kuzitatua ili ziweze kutoa mchango unaotarajiwa kwa Chama na wananchi.
Ndg. Abdi ameyasema hayo leo, Jumatano, Agosti 19, 2026, alipokuwa akizungumza baada ya kutembelea na kukagua Kituo cha Matangazo cha Bahari Media, kilichopo Migombani, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
Amesema matarajio yake ni kuona Bahari Media ikiendelea kutoa huduma bora kwa wananchi, hususan kuhakikisha taarifa zinawafikia kwa wakati na kwa ufanisi.
Aidha, amewataka watangazaji na wafanyakazi wa kituo hicho kufanya kazi kwa bidii, weledi na uwajibikaji, akisisitiza umuhimu wa utoaji wa taarifa kwa wakati na kwa kuzingatia maadili ya taaluma.
Kwa mujibu wa Ndg. Abdi, utendaji mzuri wa kituo hicho utasaidia kuongeza uaminifu kwa wadau na wahisani, jambo litakaloweza kuchochea upatikanaji wa michango na rasilimali kwa ajili ya kukiendeleza kituo hicho.
Katika ziara hiyo, Naibu Katibu Mkuu huyo aliambatana na Katibu wa NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi, Ndg. Khamis Mbeto Khamis.
Ndg. Abdi alitembelea na kukagua maeneo mbalimbali ya kituo hicho, ikiwemo studio za kurushia matangazo, chumba cha uzalishaji wa vipindi (Production), chumba cha habari (Newsroom) pamoja na maeneo mengine.
Baada ya ukaguzi, alikutana na wafanyakazi wa Bahari Media na kusikiliza maoni pamoja na changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao.
Kikao hicho kililenga kutathmini hali ya uendeshaji wa kituo, kubaini maeneo yanayohitaji maboresho na kuweka msisitizo katika hatua zinazoweza kuongeza ufanisi na kuboresha ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...