Na Mwandishi Wetu
CHUO cha Future World Vocational Institute kilichopo Chanika, Dar es Salaam, kimewahimiza wazazi kuwapeleka vijana kupata mafunzo ya ufundi yatakayowawezesha kupata ajira au kujiajiri.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 18,2026, Meneja Masoko wa chuo hicho, David Msumba, amesema mafunzo hayo yanalenga kuwapatia vijana ujuzi wa vitendo unaowawezesha kushindana katika soko la ajira na pia kuanzisha shughuli zao wenyewe.
Amesema chuo hicho kimeamua kuimarisha mafunzo ya ufundi kutokana na changamoto ya ajira inayowakabili vijana wengi wanaomaliza masomo bila kuwa na ujuzi wa moja kwa moja unaoweza kuwawezesha kujiajiri.
Msumba amesema mabadiliko katika mfumo wa elimu nchini, yanayosisitiza umuhimu wa kuunganisha elimu na ujuzi wa vitendo, yanaongeza haja kwa vijana kupata mafunzo ya ufundi ili kuwa na uwezo wa kujitegemea kiuchumi.
“Kozi hizi zinatoa fursa ya moja kwa moja ya ajira kwa vijana wetu, lakini pia zinawapa nafasi ya kujiajiri na kuanzisha shughuli zao wenyewe,” amesema Msumba.
Ameongeza chuo hicho pia kimeweka utaratibu wa malipo ya ada kwa awamu ili kuwawezesha wazazi wenye uwezo tofauti wa kifedha kuwapeleka watoto wao kupata mafunzo hayo bila mzigo wa kulipa ada yote kwa mara moja.
Kwa mfano, amesema kozi ya umeme wa majumbani inagharimu Sh950,000 kwa mwaka, ambapo mzazi anaweza kulipa kwa awamu nne.
Mbali na mafunzo, Msumba amesema chuo hicho kinatoa huduma ya hostel kwa wanafunzi wanaotoka maeneo ya mbali, hatua inayolenga kuwawezesha vijana wengi zaidi kunufaika na fursa hiyo.
Ametoa mwito kwa wazazi na vijana wa Chanika na maeneo mengine ya Dar es Salaam kutumia fursa hiyo kupata ujuzi wa ufundi utakaowawezesha kupata ajira, kujiajiri na kujenga msingi wa maisha ya kujitegemea.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...