Na Mashaka Mhando, DODOMA
KATIKA hatua ya kukuza zao la mkonge nchini na kuongeza ubora wake kwenye masoko ya ndani na nje, Serikali imetangaza mpango wa kununua mashine 10 mpya za kuchakata zao hilo (Dikotiketa/Korona) kwa ajili ya wakulima wadogo.
Sambamba na hilo, Vyama vya Ushirika (AMCOS) vitano wilayani Korogwe, vinatarajiwa kuwekeza kiasi cha Shilingi Bilioni 11.5 kupitia mikopo ya benki kwa ajili ya kusimika mitambo mipya ya kisasa ya kuchakata mkonge.
Lengo la hatua hizo ni kuhakikisha zao hilo linaendelezwa kwa tija, na kuwasaidia wananchi walioamua kulifanya mkonge kuwa zao lao kuu la biashara kupata fursa ya kuvuna na kusindika katika viwango vya ubora wa kimataifa.
Mkakati huo umetangazwa Agosti 2, 2026, na Mkuu wa Sehemu ya Maendeleo ya Mkonge kutoka Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Bw. Simon Kibasa, wakati akizungumza kwenye Maonesho ya 33 ya Kitaifa ya Kilimo (Nane Nane) yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Samwel Malecela, jijini Dodoma.
Usambazaji wa Mashine 10 za Serikali
Kibasa alieleza kuwa, uamuzi wa Serikali kununua mashine hizo 10 umekuja baada ya kubaini kuwepo kwa changamoto kubwa ya vifaa vya uchakataji kufuatia mwitikio mkubwa wa wananchi kuingia kwenye kilimo cha mkonge.
"Kati ya Korona 10 zitakazonunuliwa, tatu zimeshanunuliwa na zimewekwa Taula katika Kata ya Kwedizinga (Handeni), Mbuyuni (Mkinga), na Kijiji cha Komsala (Handeni)," alifafanua Kibasa.
Aliongeza kuwa mashine nyingine zitawekwa Makuyuni, Mswaha, na Mnazi (Korogwe); Miono (Chalinze); Kishapu (Shinyanga); Kilosa (Morogoro); na Daluni (Mkinga). Pia, Serikali kupitia TSB imekarabati mashine kwenye vituo vya Kibaranga wilayani Muheza na Lucy Estate wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Uwekezaji Mkubwa wa AMCOS
Akifunua mkakati mzito wa Vyama vya Ushirika, Kibasa alibainisha kuwa AMCOS za mashamba matano wilayani Korogwe (Ngombezi, Magoma, Mwelya, Hale na Magunga), kila moja itanunua Korona mpya kwa kuwezeshwa mikopo na mabenki.
"Kununua Korona moja mpya ni Shilingi Bilioni 1.3, na kuijengea miundombinu ni Shilingi Bilioni 1, hivyo jumla ni Shilingi Bilioni 2.3 kwa kila shamba," alieleza Kibasa, uwekezaji ambao utaleta mapinduzi makubwa ya kiviwanda wilayani humo.
Takwimu za Ukuaji na Mafanikio Chalinze
Akielezea mafanikio ya uhamasishaji uliofanywa na Serikali tangu mwaka 2019/2020, Kibasa alibainisha kuwa idadi ya wakulima wa mkonge nchini imepaa kutoka wakulima 7,551 hadi kufikia takribani 13,000 mwaka 2025/2026.
"Baada ya kuhamasisha, wakulima wengi wameingia. Mfano mzuri ni Wilaya ya Bagamoyo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze; hapo mwanzo haikuwa kabisa na wakulima wa mkonge, lakini hadi kufikia Desemba mwaka jana, tulikuwa na wakulima zaidi ya 70 ambao wanamiliki hekta zaidi ya 500," alihitimisha Kibasa, akisisitiza kuwa TSB itaendelea kusimamia ustawi wa zao hilo kikamilifu.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...