Benki ya NMB imeendelea kuifanya Nanenane 2026 kuwa zaidi ya maonesho ya kilimo kwa kuendesha kampeni ya utoaji wa elimu ya kifedha, ujasiriamali na usimamizi wa biashara kwa wananchi waliotembelea mabanda yake katika kanda mbalimbali nchini.

Katika Banda la Vijana lililopo viwanja vya DK John Mwakangale jijini Dodoma, vijana wa mradi wa Building a Better Tomorrow (BBT) walipata mafunzo kuhusu namna ya kugeuza mawazo yao kuwa biashara endelevu, kusimamia fedha na kutumia huduma za kifedha kukuza shughuli za kilimo, ufugaji na uvuvi.

 Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkuu wa Idara ya Kilimo kwa Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Christopher Mwalungenge, aliwahimiza vijana kuona kilimo kama biashara yenye fursa kubwa za kujenga kipato, ajira na ustawi wa muda mrefu.

Mbali na vijana, maafisa wa NMB waliendelea kutoa elimu kwa vikundi vya wakulima, wafugaji na wajasiriamali waliotembelea mabanda ya benki hiyo. Washiriki walipata uelewa kuhusu huduma za kifedha, mikopo ya sekta ya kilimo, bima pamoja na suluhisho zinazowawezesha kuongeza tija na kupanua biashara zao.

Kupitia elimu, ushauri na huduma za kifedha zinazotolewa katika mabanda yake, NMB imeendelea kuthibitisha nafasi yake kama mshirika wa maendeleo ya wakulima, wafugaji, wavuvi na vijana, huku ikichochea uchumi jumuishi unaojengwa kupitia maarifa na uwekezaji wenye tija. 







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...