Na Belinda Joseph-Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Stephen Michael, amesema Tanzania inalenga kuongeza uzalishaji wa maziwa na kuondokana na utegemezi wa uagizaji wa bidhaa za maziwa kutoka nje kupitia utekelezaji wa Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP).
Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 7, 2026, katika Banda la C-SDTP kwenye Maonesho ya 88 yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Malecela jijini Dodoma, Stephen amesema sekta ya maziwa ni miongoni mwa sekta muhimu zinazochangia uchumi wa nchi kupitia sekta ya mifugo.
Amesema tathmini iliyofanyika imebaini kuwa ifikapo mwaka 2030 Tanzania inaweza kukabiliwa na upatikanaji mdogo wa maziwa endapo hakutakuwa na uwekezaji wa kutosha, kutokana na kuongezeka kwa kipato cha wananchi, ongezeko la idadi ya watu na kasi ya ukuaji wa mijini.
Kwa mujibu wa Stephen, Mradi wa C-SDTP wenye thamani ya dola za Marekani milioni 231 utatekelezwa kwa kipindi cha miaka 10, ukiwa na lengo la kuongeza uzalishaji wa maziwa, kuimarisha upatikanaji wa malighafi kwa viwanda vya kusindika maziwa na kuiwezesha Tanzania kubadilika kutoka kuwa muagizaji na kuwa muuzaji wa maziwa katika masoko ya nje.
Amesema mradi huo utatumia mfumo wa corridor approach katika maeneo yenye uwezo mkubwa wa uzalishaji wa maziwa, huku ukizingatia mnyororo wa thamani wa maziwa ili kuongeza uzalishaji, ukusanyaji, usindikaji na upatikanaji wa malighafi kwa viwanda.
Ameainisha kuwa mradi utatekelezwa katika mikoa ya Arusha, Iringa, Mbeya, Njombe, Tanga, Morogoro, Pwani na Kilimanjaro kwa Tanzania Bara, huku Zanzibar ukihusisha mikoa yote mitano ambayo ni Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Kaskazini Pemba na Kusini Pemba.
Stephen amesema mradi huo pia utatoa kipaumbele kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kupitia upatikanaji wa ng’ombe bora wa maziwa kwa ruzuku, ujenzi wa vituo vya ukusanyaji wa maziwa (Milk Collection Centers na Milk Collection Points) pamoja na kuboresha miundombinu ya usafirishaji wa maziwa kutoka kwa wazalishaji kwenda viwandani.
Akizungumza Mratibu wa Mradi wa C-SDTP, Dkt. Lazaro Kapella, amesema ushiriki wa mradi katika Maonesho ya 88 ni fursa muhimu ya kukutana na wadau mbalimbali, kubadilishana uzoefu, kuonesha teknolojia na ubunifu wa ufugaji wa ng’ombe wa maziwa unaozingatia mabadiliko ya tabianchi, pamoja na kuimarisha ushirikiano katika maendeleo ya tasnia ya maziwa.
Amesema kupitia banda la C-SDTP, wananchi wanapata fursa ya kujifunza kuhusu teknolojia za uzalishaji wa malisho na lishe bora ya mifugo, huduma za afya na uboreshaji wa mifugo, ubora na usalama wa maziwa, uimarishaji wa masoko, huduma za kifedha na uwezeshaji wa vijana na wanawake.
Ameongeza kuwa mradi huo, unaotekelezwa kwa miaka 10 kuanzia 2024 hadi 2034 kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), unalenga kujenga tasnia ya maziwa yenye tija, shindani, jumuishi na endelevu, ili Tanzania iweze kuongeza uzalishaji na hatimaye kuuza maziwa katika masoko ya nje.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...