Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewataka wananchi wa Kizimkazi na maeneo ya Kusini Unguja kutunza na kudumisha miradi ya maendeleo, ikiwemo maji, afya na barabara, ili iendelee kutoa huduma bora kwa wananchi.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 14 Agosti 2026, katika kilele cha Tamasha la Kizimkazi 2026 kilichofanyika Uwanja wa Mwehe, Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema miradi hiyo ni muhimu katika kuboresha maisha ya wananchi na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii, hivyo wananchi wanapaswa kushirikiana na Serikali katika kuitunza na kuhakikisha inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesema Tamasha la Kizimkazi limeendelea kuwa jukwaa muhimu la kutangaza utalii, utamaduni na fursa za uwekezaji, kukuza vipaji, pamoja na kuwaunganisha wafanyabiashara na wajasiriamali na masoko mapya.
Ameipongeza Kamati ya Maandalizi kwa kuendelea kulikuza tamasha hilo na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono matukio yanayochangia kukuza utalii, utamaduni, biashara, ajira na kipato kwa wananchi.
Tamasha la Kizimkazi 2026 lilifunguliwa tarehe 12 Agosti 2026 na Rais Dkt. Mwinyi na kuhitimishwa leo, tarehe 14 Agosti 2026, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Uwanja wa Mwehe, Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja.







.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)


.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...