NA: MWANDISHI WETU, ZANZIBAR 

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Mary Chatanda, ameungana na viongozi na wananchi katika Tamasha la Kizimkazi katika mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Akizungumzia tamasha hilo,  Agosti 13, 2026, Chatanda amesema, linasaidia kukuza upendo, mshikamano na maendeleo miongoni mwa viongozi na wananchi, hivyo linapaswa kuendelezwa. 

"Tamasha la Kizimkazi linawaleta watu pamoja kutoka maeneo tofauti nchini, hili ni jambo kubwa sana, tunaongea na kubadilishana mawazo. Pia, miradi ya maendeleo kama ya elimu, afya, maji inazinduliwa katika kutatua kero za wananchi," amesema Chatanda

Aidha, amepongeza suala la utamaduni kuenziwa katika tamasha hilo, kwani utamaduni una umuhimu mkubwa katika kuliheshimisha taifa na kukuza maendeleo.

"Upekee mwingine wa tamasha hili ni kuenzi utamaduni wetu yaani mavazi, vyakula, ngoma za asili, lugha yetu ya Kiswahili, tukumbuke kuwa utamaduni unaibua fursa za kiuchumi katika kuongeza kasi ya maendeleo," amesisitiza.

Katika tamasha hilo, Chatanda ameshiriki uzinduzi na ukaguzi wa mradi wa Makaazi wa Amani (Amani Residency) na upandaji miti katika Kituo cha Afya Kizimkazi.

Viongozi mbalimbali wakiwemo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Dk. Hussein Mwinyi, mawaziri, wabunge, viongozi wa Chama, serikali na wananchi mbalimbali wameshiriki tamasha hilo ambalo linagusa nyanja zote za kijamii, kiuchumi na kisiasa katika kukuza maendeleo nchini.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...