TAASISI Taasisi ya Safal ALAF Foundation imepokea takriban milioni 20 kupitia safari maalumu maarufu kama The Africa Rally iliyofanyika mwaka huu ambapo washiriki waliendesha kilometa 6000 kutoka Hartbeespoort, Afrika Kusini hadi Bagamoyo, Tanzania, kuchangisha fedha kwa sababu mbalimbali.

Fedha hizo zitatumika kununua vifaa kwa ajili ya Taasisi ya Mafunzo ya Ufundi ya Safal ALAF- The Safal ALAF Technical Training Institute kupitia kampeni maalumu inayojulikana kama ‘Miles for Education’ yenye lengo ya kutoa mafunzo kwa vitendo na kutoa fursa mbalimbali za uwezeshaji kwa vijana. Taasisi hiyo ambayo ni juhudi za ALAF Limited itafungua milango kwa vijana wa kitanzania na kutoa fursa ya mafunzo ya ufundi na mafunzo stadi na kuongeza fursa za kujiajiri au kuajiriwa.

Elimu ni moja ya vipaumbele vya Safal ALAF Foundation kama njia ya kuwezesha vijana. Hii ndio sababu kuu ya ALAF kuwekeza katika taasisi hii iliyoko Arusha sanjari na uwekezaji mwingine katika jamii nchi nzima.

Tukio la mwaka huu lilihusisha washiriki 50 walioendesh amagari ya kizamani na kukatiza katika nchi tano tofauti na baadaye kuhitimisha safari hiyo Bagamoyo.

ALAF Limited’s Head of External Affairs, Ms. Hawa Bayumi, congratulated the pair on their achievement, noting that the initiative supports the development of technical skills and opportunities for young people who will enroll at the facility. “Every mile in this 6,000-kilometre journey represented commitment, resilience, and progress towards impact,” she said.

Bw. Sangeet Shah, ambaye aliiwakilisha ALAF katika tukio hilo pamoja na dereva mwenzake, Tim Pick,ambao waliendesha gari aina ya Mercedez Benz ya zamani, alisema hili kwao lilikuwa tukio la kipekee. “Lengo kuu lilikuwa ni kuchangia katika ujenzi wa Safal ALAF Technical Institute na tunafurahi kuwa tumeweza kukamilisha safari hii kikamilifu na kutimiza malengo kwani taasisi hii itawasaidia vijana wengi kutimiza malengo yao,” alisema Shah.

Alitoa wito kwa wanaopenda kuendelea kuchangia katika mfuko huo kufanya hivyo kupitia www.africarally.com kwani nafasi hiyo bado iko wazi ili kuwezesha ujenzi wa chuo hiki cha ALAF.”Tulipia pale na kujionea mradi huu wa ALAF ambao utawanufaisha watanzania wengi,” aliongeza.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa ALAF Limited, Bi. Hawa Bayumi aliwapongeza madereva hao na kuongeza kuwa jitihada zao zitasaidia katika kukuza maarifa ya kiufundi na fursa za vijana kujiunga na taasisi hiyo hapo baadaye.

“Kila maili katika safari hii ya km 6000 ilikuwa ni ishara ya kujituma, uthibiti na hatua nzuri katika kupata mafanikio mema, aliongeza.

Naye Bw. Pick alisema tukio hilo limewapa uzoefu mkubwa hasa ikizingatiwa kuwa wameshiriki ili kuchangia fedha za kuwezesha ujenzi wa chuo hicho cha ALAF.

Muandaaji wa tukio hilo maalumu, Bw. Paul Clayton aliwapongeza madereva hao kwa uamuzi wa kushiriki kwa madhumuni ya kuchangisha fedha.

“Zaidi ya Randi milioni 1.1 (Tsh milioni 173) zimekusanywa kupitia tukio hili na zitasaidia katika Nyanja mbalimbali. Chuo cha Ufundi cha ALAF kitapokea takriban Randi 119,000 (Tsh milioni 20) ambazo zinaweza kuongezeka kwani dirisha la kuchangia bado liko wazi kwa mwezi mzima kuanzia sasa,” alisema.

Alishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Bodi ya Utalii Tanzania kwa ushirikiano mkubwa walioutoa katika kufanikisha tukio hilo, ambalo lilianzishwa miaka mitano iliyopita, kumalizikia Bagamoyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...