Benki ya NMB imehitimisha ushiriki wake katika Tamasha la Kizimkazi 2026 kwa kuunganisha wananchi na huduma za kifedha pamoja na fursa za kukuza biashara.

NMB ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa tamasha hilo lililofikia kilele jana, Agosti 14, Kusini Unguja. Banda la benki hiyo lilitumika kutoa elimu ya fedha na kueleza huduma zinazolenga wafanyabiashara, wajasiriamali na wananchi wa Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alipotembelea banda hilo, alipokea maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Biashara za Serikali wa NMB, Vicky Bishubo, kuhusu ushiriki wa benki katika tamasha na huduma ilizopeleka kwa wananchi.

Ushiriki huo umeimarisha nafasi ya Kizimkazi kama jukwaa la kutangaza fursa za kiuchumi, kuibua biashara na kuleta huduma muhimu karibu na jamii.

PICHA 1: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwakilishi wa Idara ya Biashara za Serikali wa Benki ya NMB, Vicky Bishubo, alipotembelea banda la benki hiyo katika Tamasha la Kizimkazi 2026, Zanzibar. NMB ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa tamasha hilo lililofikia kilele jana.



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi cheti cha kutambua ushiriki wa NMB katika kufanikisha Tamasha la Kizimkazi 2026 kwa mwakilishi wa benki hiyo.






Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...