Serikali mkoani Geita kupitia tume ya umwagiliaji  imesambaza jumla ya pampu 141 za umwagiliaji kwa vikundi 119 vya wakulima wenye takribani wanachama 13,000 katika halmashauri zote za mkoa huo, katika jitihada za kuongeza uzalishaji na kupunguza utegemezi wa mvua.

Akikabidhi pampu hizo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Paskas Muragili amesema pampu hizo zitaleta kasi kubwa ya uzalishaji kwa wakulima na kuchangia katika mapinduzi ya kilimo mkoani humo.

Ameongeza kuwa ugawaji wa pampu hizo unapaswa kwenda sambamba na ushirikishwaji wa sekta nyingine ikiwemo utoaji wa elimu na mbinu bora za kilimo na pia uhakikishaji wa upatikanaji wa pembejeo kwa wakati.

Kwa upande wake Mhandisi kutoka Timu ya Umwagiliaji mkoa wa Geita, Boniface Mkita amesema pampu hizo zimegharimu jumla ya shilingi bilioni 1.012.

Amefafanua kuwa kupitia mpango huu, eneo lenye ukubwa wa hekari 2,092 litamwagiliwa kwa wakati mmoja. Hii itapunguza utegemezi wa mvua na kupandisha uzalishaji wa zao la mahindi kutoka tni 1 kwa hekari hadi tani 2.5 kwa hekari1 

Mkita amebainisha kuwa mpango huu unatarajiwa kuwanufaisha moja kwa moja wakulima 1,389, kati yao wanawake 369 na wanaume 1,020.

 Serikali imesisitiza kuwa uwekezaji huu ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha Geita inakuwa miongoni mwa mikoa inayolisha Taifa kupitia kilimo cha umwagiliaji.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...