Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) inashiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2026, yanayofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, mkoani Tanga.
Maadhimisho hayo yameanza leo, Agosti 15, 2026, na yanatarajiwa kuhitimishwa Agosti 24, 2026, yakibeba kaulimbiu isemayo: “Elimu, Ujuzi na Ubunifu, Njia ya Kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.”
Katika maadhimisho hayo, wadau mbalimbali wa sekta ya elimu, ujuzi, sayansi, teknolojia na ubunifu wameendelea kujitokeza kushiriki na kuonesha mchango wao katika maendeleo ya taifa.
Miongoni mwa viongozi walioshiriki ni Mkurugenzi wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Ladslaus Mnyone.
Maadhimisho hayo yamewakutanisha zaidi ya taasisi 100 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, zikiwa na lengo la kuonesha bunifu, ujuzi na fursa mbalimbali zinazoweza kuchangia katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.


.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...