Vodacom Tanzania kupitia Vodacom Tanzania Foundation inaendelea kuchangia uboreshaji wa mazingira ya kujifunzia kwa watoto kupitia ukarabati na ujenzi wa madarasa katika shule tatu za msingi za umma zilizopo Pwani, Ruvuma na Morogoro.
Mpango huu, unaotekelezwa kwa kuzingatia mahitaji yaliyobainika, unalenga zaidi kusaidia watoto wenye mahitaji maalum katika shule za umma. Kupitia mpango huu, madarasa sita yamefanyiwa maboresho, ambapo shule za msingi Vikindu - Mkuranga, Mahilo - Songea na Ihowanja - Morogoro zimepatiwa madarasa mawili kila shule.. Kati ya madarasa hayo, mawili yamekarabatiwa na manne yamejengwa upya. Maboresho haya yanatarajiwa kuwafikia wanafunzi 4,838, wakiwemo 117 wenye mahitaji maalum, pamoja na walimu 52, sambamba na utoaji wa madawati 90 kwa shule zote tatu.
Hafla ya kwanza ya makabidhiano hayo ilifanyika katika Shule ya Msingi Vikindu, Wilaya ya Mkuranga, ambapo Vodacom Tanzania ilikabidhi madarasa pamoja na madawati hayo. Mpango huo utaendelea katika Shule ya Msingi Mahilo mkoani Ruvuma, tarehe 20 Agosti 2026 na Shule ya Msingi Ihowanja, Morogoro, tarehe 27 Agosti 2026.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano katika Shule ya Msingi Vikindu, George Nyanda, Meneja Mauzo Kanda ya Dar es Salaam na Pwani wa kampuni ya Vodacom Tanzania alisema, “katika Shule ya Msingi Vikindu, madarasa haya mawili yanalenga kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto na kufundishia kwa walimu. Kuitikia mahitaji ya jamii kunahitaji kuelewa mambo yanayoweza kuleta tofauti katika maisha ya kila siku ya watoto, hususan wale wenye mahitaji maalum. Tunafurahi kuchangia katika kuweka mazingira ambayo yatawawezesha wanafunzi kujifunza kwa utulivu na kujisikia kuwa sehemu ya jamii ya shule.”
Akizungumzia msaada huo katika Shule ya Msingi Ihowanja, Chiha Nchimbi, Mkuu wa Kanda ya Kati wa kampuni hiyo aliongeza, “katika Shule ya Msingi Ihowanja, madarasa haya mawili mapya yanaongeza nafasi muhimu za kujifunzia kwa jamii ya shule. Haya ni maeneo ambayo yatatumika kila siku kwa ajili ya masomo, kukuza ujuzi na kuwawezesha watoto kuendelea kujifunza na kukua. Haya ndiyo mahitaji ya jamii ambayo Vodacom Tanzania Foundation inalenga kuyaitikia kupitia mipango yake.”
Kuhusu namna msaada huo utakavyoleta neema katika Shule ya Msingi Mahilo, Mkuu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa Vodacom Tanzania, Abednego Mhagama alifafanua, “katika Shule ya Msingi Mahilo, madarasa haya mawili mapya yatawapatia wanafunzi na walimu mazingira bora zaidi ya kujifunzia na kufundishia. Darasa si jengo pekee; ni sehemu ambayo watoto hutumia muda wao mwingi kujifunza na kujiandaa kwa maisha yao ya baadaye. Tunafurahi kuchangia katika kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa jamii hii.”
Maboresho haya ya madarasa ni sehemu ya mchango unaoendelea wa Vodacom Tanzania Foundation katika kusaidia elimu na kuboresha mazingira ya kujifunzia katika jamii mbalimbali nchini, kwa kuzingatia mahitaji yaliyobainika. Foundation imewahi kusaidia mipango kama hii hapo awali na inaendelea kuelekeza juhudi zake katika maeneo yenye mahitaji.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mkuranga Helen Kulwa Benjamini (kushoto) akishikana mkono na Meneja Mauzo Mwandamizi wa Kanda ya Dar es salaam na Pwani wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc George Nyanda (kulia) wakati wa makabidhiano ya madarasa mawili yaliyoboreshwa pamoja na madawati 30 katika shule ya msingi Vikindu chini ya mpango wa kampuni hiyo wa kurejesha kwa jamii yaliyofanyika kwa lengo la kuwajengea wanafunzi wa shule ya msingi mazingira bora ya kujifunzia. Hafla hiyo limefanyika tarehe 14 Agosti 2026, Vikindu, Mkoani Pwani.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mkuranga Madam Helen Kulwa Benjamini (kulia) akishikana mkono na Meneja Mauzo Mwandamizi wa Kanda ya Dar es salaam na Pwani wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc George Nyanda (kushoto) wakati wa makabidhiano ya madarasa mawili yaliyorekebishwa pamoja na madawati 30 yaliyotolewa na Kampuni hiyo. Tukio hilo lilishuhudiwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Vikindu Said Nguvumari (kulia) na Mwenyekiti wa CCM kata ya Vikindu Bahati Ali Mawinga.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye moja ya darasa lililofanyiwa marekebisho katika shule ya msingi vikindu.





.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...