Na Janeth Raphael - MichuziTv
Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 ya kujenga Tanzania yenye uchumi wa kisasa, jamii yenye ustawi, huduma bora za kijamii pamoja na matumizi makubwa ya teknolojia na ubunifu, imeelezwa kuwa inahitaji Serikali za Mitaa imara, zenye uwezo na zinazowajibika ili kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa kwa ufanisi na kwa usawa.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Dkt. Jafar Seif, amesema ugatuzi wa madaraka katika mamlaka za Serikali za Mitaa ni nyenzo muhimu ya kufanikisha Dira hiyo, kwa kuwa unawawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika maamuzi na utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
Dkt. Seif ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 16 wa Taasisi ya Maboresho katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA), unaofanyika chini ya kaulimbiu isemayo “Ugatuzi wa Madaraka katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ni Nyenzo Madhubuti ya Kufikia Dira ya Taifa 2050.”
Amesema ugatuzi wa madaraka si suala la kiutawala pekee, bali ni msingi wa kuwapa wananchi nafasi ya kushiriki katika maamuzi yanayohusu maendeleo yao, akieleza kuwa Serikali za Mitaa ndizo zilizo karibu zaidi na wananchi na zina nafasi kubwa katika kuhakikisha huduma na miradi ya maendeleo inawafikia kwa wakati.
“Serikali za Mitaa zikiwa imara na zenye uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, Taifa linaweza kufikia malengo yake kwa haraka zaidi na kwa usawa,” amesema Dkt. Seif.
Amesema Serikali imepanga kuchukua hatua zaidi katika eneo la ugatuzi wa madaraka kwa kuimarisha mifumo mbalimbali ya kiutendaji na usimamizi, hususan katika eneo la fedha, hatua inayolenga kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa miradi na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Dkt. Seif amesema kwa sasa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo zinapelekwa moja kwa moja katika taasisi za Serikali zilizopo ngazi za chini, ikiwemo shule, zahanati, ofisi za kata, vijiji pamoja na maeneo mengine ya kiutawala na kiutendaji.
Ameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kuhakikisha rasilimali zinazotengwa kwa ajili ya maendeleo zinawafikia walengwa moja kwa moja na kutumika katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao.
Aidha, Dkt. Seif amesema ili Dira ya Taifa ya 2050 ifikiwe, Serikali za Mitaa zinapaswa kuimarisha maeneo muhimu ikiwemo uongozi bora na uwajibikaji, mipango madhubuti ya maendeleo, usimamizi wa rasilimali za umma, ushirikishwaji wa wananchi pamoja na matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma.
Amesema TOA imeendelea kuwa jukwaa muhimu la kuwakutanisha viongozi na wataalamu wa Serikali za Mitaa kwa ajili ya kubadilishana uzoefu, kujifunza na kutafuta suluhisho la changamoto zinazojitokeza katika ngazi za chini za utendaji.
Dkt. Seif amesisitiza kuwa mafanikio ya ugatuzi wa madaraka yanategemea kwa kiasi kikubwa uwezo wa taasisi kujenga mazingira ya uwazi, uwajibikaji na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya Serikali za Mitaa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TOA, Albert Msovela, amesema taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali katika kusimamia maendeleo ya wananchi na kuimarisha utawala bora, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kujenga uwezo wa mamlaka za Serikali za Mitaa ili ziweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Mkutano huo wa 16 wa TOA unajadili masuala mbalimbali yanayohusu maboresho ya utendaji wa Serikali za Mitaa, ugatuzi wa madaraka na namna ya kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi katika kuelekea utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...