Farida Mangube, Morogoro
Tanzania imepiga hatua katika kuelekea kujitosheleza kwa sukari kufuatia kuanza rasmi kwa uzalishaji katika Kiwanda kipya cha Kisasa cha Sukari Kilombero K4 kilichopo mkoani Morogoro, ambacho kimegharimu zaidi ya shilingi bilioni 700.
Uwekezaji huo unatarajiwa kuongeza uzalishaji wa sukari nchini, kupunguza utegemezi wa uagizaji kutoka nje na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Akizungumza katika maonesho ya nanenane Kanda ya Mashariki Mkurugenzi wa Biashara wa Kiwanda cha Sukari Kilombero, Fimbo Butallah, amesema kuanza kwa uzalishaji katika kiwanda hicho kutasaidia kuziba pengo la upungufu wa sukari nchini na kuongeza upatikanaji wa bidhaa hiyo kwa wananchi.
Butallah amesema pia kiwanda hicho kimezingatia tofauti za vipato vya Watanzania kwa kuzalisha sukari katika ujazo wa aina mbalimbali, hatua itakayowezesha wananchi kupata bidhaa hiyo kulingana na uwezo wao wa kifedha.
Kwa upande wake, Meneja wa Ufuatiliaji na Uthibitishaji kutoka Bodi ya Sukari Tanzania, Bahati Hakimu, amesema kukamilika kwa Kiwanda cha Kilombero K4 ni hatua muhimu katika kuongeza uzalishaji wa sukari nchini, huku pia kikitarajiwa kuongeza ajira kwa wakulima wa miwa na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika Bonde la Kilombero.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...