WADAU wote wa lishe wa Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa wametakiwa kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa elimu ya lishe unaotolewa katika jamii na kuhakikisha ubora wa vyakula vinavyozalishwa unachangia kuboresha afya za watumiaji na kupunguza tatizo la udumavu.

Kauli hiyo imetolewa leo Aug 19, 2026 na kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Nassir Kirusha wakati akifungua kikao cha kamati Jumuishi ya Lishe cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026, kilicholenga kutathimini utekelezaji wa kuboresha Lishe na kuimarisha mikakati ya kukabiliana na udumavu katika Manispaa ya Sumbawanga.

Kirusha amesema ni muhimu kuhakikisha upatikanaji wa lishe bora kwa makundi yote, kuongeza uzalishaji wa vyakula vya kutosha na ubora ili  kuvitumia kwa mlo kamili kila siku pamoja na kuimarisha utekelezaji wa afua za lishe na kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Amesisitiza kuwa uhamasishaji wa matumizi ya chakula bora na mlo kamili ni nguzo muhimu katika kuzuia udumavu, hivyo kuwawezesha Wananchi kuwa na afya njema na kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji kwa maendeleo yao na Jamii kwa ujumla. 

Aidha ametoa wito wa kuzingatia matumizi ya vyakula vyenye virutubisho vya kutosha ili kuimarisha Ustawi wa Wananchi.

Kwa upande wa utekelezaji, Kamati ya Lishe ya Manispaa ya Sumbawanga imefanikiwa kutoa elimu ya lishe kwa Wananchi, kuanzisha klabu za lishe katika shule zote za Msingi na Sekondari 107 za Manispaa ya Sumbawang sawa na asilimia 100 pamoja na kuendelea na ufuatiliaji wa hali ya lishe shuleni.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...