Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Benki ya Dunia katika kuimarisha sekta za elimu, afya, nishati na miundombinu, huku akisisitiza kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili wananchi wanufaike kwa wakati.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 19 Agosti 2026, alipokutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Ndiamé Diop, aliyeambatana na Mkurugenzi wa Divisheni ya Benki hiyo anayesimamia Malawi, Tanzania, Zambia na Zimbabwe, Bw. Firas Raad, katika mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Zanzibar. Miongoni mwa waliohudhuria mazungumzo hayo ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ndg. Khamis Abdulla Said, pamoja na viongozi na watendaji wengine wa Serikali na Benki ya Dunia.
Amesema Serikali itaendelea kuimarisha uwekezaji katika sekta za kipaumbele, kutoa fursa kwa Sekta Binafsi na kuimarisha mafunzo ya amali ili vijana wapate ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira.
Kwa upande wake, Dkt. Ndiamé Diop amesema Benki ya Dunia imeridhishwa na kasi ya maendeleo Zanzibar na itaendelea kushirikiana na Serikali katika maeneo yenye vipaumbele vya pamoja.



.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...