Jane Mwakyoma,Rukwa.

MAADHIMISHO ya nane nane mwaka 2026 yamefunguliwa leo Aug 1, katika mamlaka ya mji mdogo wa Laela Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa na yatafikia kilele chake Aug 8 mwaka huu,huku maadhimisho hayo yakibeba kauli mbiu ya mwaka huu "Tambua soko,ongeza tija kutekeleza Dira 20250".

Halmashauri hiyo inaadhimisha sikuku hiyo ndani ya wilaya yake kwa kutambua umuhimu wa kilimo kinachotegemewa na wakazi wa wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla,ambapo maadhimisho hayo yanaambatana na utoaji wa elimu ya kilimo cha kisasa kwa wananchi,ikiwa maadhimisho hayo kwa mikoa ya nyanda za juu kusini yanaadhimishwa jijini Mbeya.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi waliofika katika maonyesho hayo,wamepongeza uongozi wa Halmashauri hiyo kwa kuweka maadhimisho ya sikuku ya nane nane ndani ya wilaya yao na kuwa maadhimisho hayo yanatoa frusa kwa wakulima kujifunza mbegu mpya na zenye tija pamoja na kupata elimu ya kilimo cha kisasa na kitakacholeta matokeo chanya kwa wakulima.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Nyakia Chirukile amesema lengo la kuweka maadhimisho hayo katika wilaya hiyo ni kutoa elimu ya kilimo kwa wananchi ili waweze kujifunza matumizi bora ya bembejeo za kilimo zitakazowasaidia wakulima kuinuka kiuchumi.

Aidha amewataka wananchi wa wilaya hiyo kutumia frusa ya maonyesho hayo kupata elimu ya kilimo itakayowasaidia kutoka katika kulima kilimo cha mazoea na kujikita katika kilimo cha kisasa na chenye tija ili kukuza uchumi wao.

Pia ameyataka makampuni yanayosambaza pembejeo za kilimo kutoa elimu sahihi na kuzitolea ufafanuzi mbegu na mbolea zinazofaa katika ukanda huo na kuzingatia utaalamu wa kilimo utakaokuwa na manufaa kwa wakulima wa wilaya hiyo.

Naye Afisa lishe wa Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga Alphani Mwani amesema maonyesho hayo ni muhimu kuendelea kuwepo kila mwaka na wananchi wapate elimu ya kilimo pamoja na elimu ya lishe ili kujenga jamii yenye afya.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...