Jane Mwakyoma, Aug1,2026, Rukwa.
JESHI la Polisi Wilayani Nkasi mkoani Rukwa limetoa misaada ya mahitaji mbalimbali kwa wazee 30 wasiojiweza ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uhusiano kati ya Jeshi la Polisi na jamii pamoja na kuendeleza utamaduni wa kuwajali makundi yenye uhitaji maalumu.
Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Shadrack Masija amesema Jeshi la Polisi lina wajibu wa kulinda usalama wa raia na mali zao na linaendelea kutekeleza shughuli za kijamii zinazolenga kugusa maisha ya wananchi, hususan wazee wasiojiweza.
Amesema hatua hiyo ni sehemu ya falsafa ya Polisi Jamii inayohimiza ushirikiano, mshikamano na kuwajali wananchi katika nyanja mbalimbali za maisha, huku akitoa wito kwa wadau na jamii kuendelea kuwaunga mkono wazee na makundi mengine yenye mahitaji maalumu.
Kwa niaba ya maafisa wakaguzi na askari wa Wilaya ya Nkasi, Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo, Wenceslaus Gumha amesema misaada hiyo ni ishara ya upendo na kuthamini mchango wa wazee katika jamii, akibainisha kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kushiriki shughuli za kijamii zinazolenga kuimarisha ustawi wa wananchi.
Misaada iliyotolewa imejumuisha blanketi, vitenge, unga, sukari pamoja na mahitaji mengine muhimu ya matumizi ya kila siku ili kuwasaidia wazee hao kukabiliana na changamoto za maisha.
Kwa upande wao, wananchi waliohudhuria hafla hiyo katika viwanja vya Polisi Wilaya ya Nkasi pamoja na wazee walionufaika wamelishukuru Jeshi la Polisi kwa moyo wa kujitolea na kuwajali wenye uhitaji kuwa hatua hiyo imeonyesha kuwa Polisi si walinzi wa usalama pekee bali pia ni wadau wa maendeleo na ustawi wa jamii.
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...