Miaka tisa baada ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa mara ya kwanza, mtangazaji wa redio Willy Nkya amepanda tena mlima huo, safari hii akiwa na jukumu la kuripoti matukio kila siku akiwa katika kilele cha mlima huo.
Nkya, ambaye alipanda mlima Kilimanjaro kwa mara ya kwanza mwaka 2017 muda mfupi baada ya kumaliza chuo, anasema safari yake ya mwaka huu imekuwa ya tofauti kwa namna kadhaa. Amepanda mlima akiwa na uzoefu zaidi akiwa na maandalizi ya kutosha ya mwili na uelewa mzuri wa namna ya kukabiliana na uchovu, baridi na mabadiliko ya hali ya hewa kadri anavyopanda.
Tofauti nyingine kubwa ilikuwa mawasiliano; safari hii ameweza kuwasiliana na kutekeleza majukumu yake ya kikazi katika maeneo mengi ya mlima.
Akiwa katika safari hiyo, alitakiwa kurekodi na kutuma video, sauti, picha na taarifa mbalimbali kwa ajili ya matangazo ya redio na mitandao ya kijamii.
Anasema mtandao wa Viwango wa Yas ulimwezesha kuendelea kutekeleza majukumu yake katika maeneo mengi aliyopita kuelekea kileleni, huku pia akiendelea kuwasiliana na familia na marafiki.
“Tofauti na mwaka 2017 ambapo mawasiliano yalikua ni ya shida, safari hii mambo yalikua ni tofauti, nimeweza kutuma video, picha, sauti na kuwasiliana bila matatizo na watu wangu wa karibu,” anasema Nkya.
“Kupanda mlima Kilimanjaro si mchezo. Kuna wakati unahisi kabisa uko kwenye dunia nyingine. Mtandao wa viwango wa Yas ambao unapatikana vizuri kabisa katika maeneo mengi ya mlima tuliyopita umenisaidia kuendelea kutimiza majukumu ya kazi zangu bila shida.” anasema.
Nkya aliendelea na safari hiyo hadi kufika Uhuru Peak, mita 5,895 kutoka usawa wa bahari, kilele cha juu zaidi barani Afrika.
Anasema safari yake ya mwaka huu imempa picha tofauti na ile ya miaka tisa iliyopita, hasa kwa namna ambavyo mawasiliano yalivyorahisisha mambo mengi katika mazingira ya mlima huo wenye changamoto nyingi.
“Kwangu hii ndiyo maana ya Mtandao wa Viwango, mtandao unaokuwezesha kuendelea kufanya kile unachotaka kufanya hata ukiwa katika safari yenye changamoto. Nimepanda na Yas hadi Uhuru Peak na nimeendelea kuwasiliana na dunia,” anasema.
Kwa Nkya, kufika Uhuru Peak hakukuwa mwisho wa safari pekee, bali pia ujumbe kwamba kila mtu ana kilele anachotamani kukifikia.
“Kila mmoja wetu ana kilele anachopanda katika maisha yake. Cha kwangu safari hii kilikuwa Uhuru Peak.”

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...