NA MWANDISHI WETU
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema watu 51 wamehukumiwa na Mahakama ya Jiji la Dar es salaam, kwenda jela kutokana na kujihusha na vitendo vya uchafu.
Ameyasema hayo alipoongoza wananchi kufanya usafi katika mitaa mbalimbali wilayani humo na kueleza wataendelea kusimamia sheria ndogo kuwabana wananchi wote wasiozingatia kanuni za usafi.
"Kikosi kazi chetu kinaendelea kufanya kazi ya kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuzingatia usafi. Tayari kimewapitia watu zaidi ya 500. Watu watu 340 walionywa," amesema Mpogolo.
Mkuu huyo wa wilaya ameeleza, watu 191 walipata adhabu mbalimbali, kati yao 19 walitozwa faini ya papo kwa papo.
Mpogolo amebainisha kwa mujibu wa sheria hizo ndogo za usafi faini inayotozwa ni kuanzia sh.300,000 hadi sh.1,000,000.
"Waliopelekwa mahakamani na kuhukumiwa kisha kulipa fani ni watu 121 na waliofungwa na kwenda kutumikia kifungo jela ni watu 51,"amesema Mpogolo.
Amesisitiza wananchi kuzingatia kanuni za usafi na wale wote watakao kiuka watachukuliwa hatua ikiwemo kukamatwa, kutozwa faini , kufikishwa mahakamani ambako wakipatikana na hatia sheria inaelekeza kutozwa faini kuanzia sh. 300,000 hadi sh.1,000,000 au kifungo cha mwaka mmoja hadi miwili au vyote kwa pamoja.
Ameeleza ni marufuku mwananchi kutupa taka hovyo, hususan chupa za maji au juisi, bifungashio vya vitafunwa mbalimbali na kusisitiza magari, maduka, ofisi ,mitaa, magari na nyumba zote kuwa na vifaa vya kuhifadhia taka.
Aidha Mpogolo, amepiga marufuku wafanyabiashara wa Soko la Karume kupanga bidhaa zao katika Barabara ya Uhuru na atakaye kiuka atachukuliwa hatua.
Alielekeza Polisi wilayani humo kuhakikisha barabara katika eneo hilo inapitika wakati wote baada ya ujenzi wa miundombinu ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) kukamilika.
"Tufunge sasa magari kutumia njia za mwendo kasi katika eneo hili. Magari yaanze kutumia barabara hii ya kawaida. Biashara zote ziingie ndani ya maduka,"ameeleza.
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amepokea vifaa vya usafi vilivyotolewa na Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) ikiwa ni hatua ya wakala huo kuunga mkono kampeni ya usafi wilayani humo.
Ameomba taasisi zingine, watu binafsi na vikundi kuendelea kujitokeza kutoa msaada wa vifaa hivyo pamoja na kushiriki kufanya usafi.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, ambaye pia ni Mwanasheria wa jiji hilo, Faraja Nakua, amesema wataalamu na vijana waliohitimu Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wanaendelea kusimamia sheria katika kata zote za jiji hilo, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya usafi.
Amesema halmashauri hiyo imekusanya sh.milioni 52.5 kutokana na utozaji wa faini na kwamba wiki ijayo kasi itaongezwa hususan elimu,makalipio na utozaji wa faini kwa mujibu wa sheria.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...