NA DENIS MLOWE, IRINGA.

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Salim Abri Asas, ametunukiwa tuzo maalumu ya heshima katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Mkoa wa Iringa, kwa kutambua mchango wake katika shughuli za Chama na jitihada za kukiimarisha.

Tuzo hiyo imetolewa baada ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Iringa kuwasilisha hoja ya kutambua mchango wa Asas, ambayo baadaye iliwasilishwa katika Mkutano Mkuu Maalum na kupata ridhaa ya wajumbe wa mkutano huo.

Miongoni mwa sababu zilizozingatiwa katika kumpatia tuzo hiyo ni mchango na msaada anaoutoa katika shughuli mbalimbali za CCM, pamoja na kujitolea katika ujenzi wa ofisi za Chama katika ngazi ya Kata katika Mkoa wa Iringa.

Tuzo hiyo imekabidhiwa na Katibu wa NEC, Idara ya Oganaizesheni, Paul Matiko Chacha (MCC), katika mkutano uliofanyika katika Chuo cha UVCCM Ihemi, Iringa, mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum.

Akizungumza kabla ya kupokea tuzo hiyo, Asas amesema viongozi wanapaswa kujenga alama chanya kupitia matendo yao ndani ya Chama, akisisitiza umuhimu wa kila mmoja kujiuliza mchango anaouacha katika kukijenga na kukiimarisha CCM na sio chama kimemfanyia nini.

Asas amesema ana dhamira ya kuona kila Kata inakuwa na Ofisi ya CCM, akieleza kuwa juhudi za kuhakikisha ofisi hizo zinajengwa zinapaswa kuendelea hata baada ya yeye kutokuwepo, ili malengo hayo yaweze kutimia na kuwaachia familia maagizo hata kama hay hayupo duniani.

Amesema ujenzi wa ofisi za CCM katika ngazi ya Kata ni sehemu ya mchango wa wanachama katika kukiimarisha Chama na kuweka mazingira bora ya utekelezaji wa shughuli zake.

Tuzo hiyo imekuja wakati CCM Mkoa wa Iringa ukiendelea kuhimiza ushiriki na kujitolea kwa wanachama katika kuimarisha miundombinu ya Chama, hususan ujenzi wa ofisi katika ngazi ya Kata.ambazo amewahakikishia zitajengwa kila kata.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...