Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Ndugu Abdi Mahamoud Abdi, amesema ameridhishwa na uimara wa Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Donge, akisema hali hiyo inaonesha umoja na mshikamano uliopo miongoni mwa viongozi na wanachama wa chama hicho.
Ndugu Abdi ameyasema hayo mara baada ya kuwasili katika Tawi la CCM Njia ya Mtoni, Jimbo la Donge, ambako aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa tawi hilo, ikiwa ni sehemu ya ziara zake za kukagua na kuimarisha uhai wa Chama Cha Mapinduzi katika matawi mbalimbali.
Amesema umoja na mshikamano unaoonekana katika Jimbo la Donge ni mfano unaopaswa kuigwa na majimbo mengine, huku akisisitiza kuwa mshikamano miongoni mwa viongozi na wanachama ni msingi muhimu katika kukiimarisha na kukiendeleza chama.
Kwa upande wake, Katibu wa Uchumi na Fedha kutoka Afisi Kuu ya CCM Zanzibar, Ndugu Afadhali Taibu Afadhali, amewapongeza wanachama wa CCM Jimbo la Donge kwa kukipa ushindi chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Ndugu Afadhali amewataka viongozi na wanachama wa CCM kuendelea kuhamasishana kuhusu ulipaji wa ada za uanachama, akisema hatua hiyo ni miongoni mwa mambo muhimu yanayokiwezesha chama kujiendesha na kuendelea kuwa imara.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa vikao vya matawi kufanyika mara kwa mara ili kujadili changamoto zinazowakabili wanachama, kuzitafutia ufumbuzi na kuhakikisha utekelezaji wa maamuzi unafanyika kwa wakati.
Katika kuendeleza utamaduni wa kujenga mshikamano na kujali viongozi na wanachama, Ndugu Abdi pia aliwatembelea na kuwajulia hali wazee wa chama, akiwemo Katibu Mstaafu wa UWT Tawi la Mto wa Pwani, Ndugu Tatu Hamdani Muhidini, nyumbani kwake Mtambile.
Pia alimtembelea Katibu wa Baraza la Wazee Jimbo la Mahonda, Ndugu Salma Kassim Iddi, ikiwa ni sehemu ya ziara hiyo yenye lengo la kuimarisha mshikamano, upendo na kujali hali za viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...