Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Ndugu Abdi Mahamoud Abdi, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeendelea kuboresha mazingira ya wafanyabiashara na wavuvi ili kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi na kuongeza fursa za kiuchumi.

Ndugu Abdi ameyasema hayo leo, Septemba 17, 2026, wakati akikagua ujenzi wa Mradi wa Diko Fungurefu, ambapo amesema CCM imeridhishwa na hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa mradi huo.

Amesema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kuboresha mazingira ya biashara, kuimarisha shughuli za uvuvi na kuongeza fursa za kiuchumi kwa wananchi, hususan wafanyabiashara na wavuvi.

Ameeleza kuwa ujenzi wa mradi huo ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuendelea kuwaletea maendeleo wananchi na kuboresha mazingira ya shughuli zao za kila siku.

📆 17 Septemba, 2026
📍 Fungurefu, Zanzibar








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...