JESHI la polisi mkoani Rukwa linamshikilia Maiko Sosolo Kazikulima (35) mkazi wa Kijiji Cha Mashete kata ya Mashete wilayani Nkasi mkoan Rukwa kwa tuhuma za kumuua mkewe  Victoria Mputa  (32) kwa kumpiga kichwani  akimtuhumu mkewe kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume wengine.

‎Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kamanda wa polisi mkoa Rukwa SACP Shadrack Masija amesema tukio hilo limetokea Jana J,Nne September 8,2026 majira ya saa 3 usiku wakati wakitoka kilabuni pamoja, ndipo ulipozuka ugomvi miongoni mwao uliohusishwa na wivu wa kimapenzi na kusababisha kuuawa kwa mwanamke huyo.

‎Amefafanua kuwa mtuhumiwa ambaye alikua mume wa marehemu wakiwa njiani kabla hawajafika nyumbani mzozo mkubwa kati Yao uliibuka huku Mume akiendelea  kumtuhumu mkewe kwa kuwa na mahusiano mengine na Wanaume wengine kiasi Cha kuchukua maamuzi ya kuanza kumpiga na rungu kichwani  kinyume Cha Sheria.

‎Kamanda Masija amesema mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na Polisi na kuwa upelelezi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.

‎‎Sambamba na hilo amewataka Wananchi kuendelea Kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi katika kuwabaini wahalifu na kuwa katika kipindi hiki wamekua wakipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Wananchi kitu kilichopelekea wahalifu wengi kunaswa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...