Wanakijiji wa Kinyamwenda, Kata ya Itaja, Wilaya ya Singida, wamepongeza ujenzi wa birika la kunyweshea punda na mifugo lililojengwa na INADES-Formation Tanzania kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Singida na wananchi, kwa ufadhili wa Brooke East Africa.
Birika hilo lilizinduliwa leo na Nathalia Mosha, Afisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, ambaye alisema linatarajiwa kuwahudumia takribani punda 720 na zaidi ya mifugo 9,000 kutoka Kinyamwenda na vijiji jirani vya Mipilo, Mwighanji na Itaja.
Mosha aliipongeza INADES-Formation Tanzania kwa kuleta mradi wa kuboresha maisha ya jamii kupitia ustawi wa mnyama kazi pundakatika vijiji vya Kinyamwenda, Ghata na Endesh, akisisitiza kuwa kuboresha ustawi wa punda kuna mchango mkubwa katika kuboresha maisha ya jamii zinazowategemea.
Aliwataka wananchi waliopatiwa mafunzo kuhusu ustawi wa punda kuendelea kutoa elimu kwa wengine, hususan kuhusu matumizi sahihi ya tandiko na nira, ili kuwalinda punda dhidi ya majeraha na maumivu yasiyo ya lazima.
Akizungumza katika hafla hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa INADES-Formation Tanzania, Jacqueline Nicodemus, Mkuu wa Idara ya Mafunzo, Michael Kihwele, aliwapongeza wananchi kwa ushirikiano wao katika kufanikisha ujenzi wa birika hilo “Punda anapoboreka, nayo maisha ya jamii yataboreka kupitia mradi huo,” alisema Kihwele.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa la Utetezi na Ustawi wa Punda Wilaya ya Singida, Wilfred Mande, alisema birika hilo litapunguza umbali mrefu ambao mifugo imekuwa ikitembea kutafuta maji, hivyo kuimarisha ustawi wa punda na mifugo mingine.
Mande pia alieleza kuwa mradi huo umechangia kupungua kwa ukatili dhidi ya punda, kuimarika kwa huduma za afya kupitia kliniki za punda, kuanzishwa kwa klabu za ustawi wa punda shuleni, pamoja na kuwawezesha vikundi vya wananchi katika ujasiriamali, kuweka na kukopa.
Alisema vikundi pia vimeanza kutenga fedha kwa ajili ya kliniki za punda zinazofanyika kila baada ya miezi mitatu, hatua inayosaidia kuhakikisha punda wanapata matibabu na kutambuliwa kama wanyama wenye mchango mkubwa katika maisha ya jamii.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...