Mkoa wa Geita ukiwa ni miongoni mwa maeneo yenye shughuli kubwa za madini nchini, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeeleza kuwa uwepo wa shughuli hizo unaendana na mzunguko mkubwa wa fedha, hivyo ni muhimu kwa wananchi na watoa huduma za fedha kuhakikisha fedha hizo zinawekwa na kuzunguka kupitia mifumo na taasisi za fedha zilizo salama na zinazotambuliwa kisheria.
Akizungumza na Michuzi TV Septemba 28, 2026 katika mwendelezo wa Maonesho ya 9 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita, Afisa Mkuu Mwandamizi kutoka Benki Kuu ya Tanzania, Mwile Kauzeli, amesema mtu anayetaka kufanya shughuli za huduma ndogo za fedha anapaswa kufika Benki Kuu kwa ajili ya kupata maelekezo na kutimiza utaratibu wa kupata leseni.
Amesema mwombaji wa leseni anatakiwa kuwa na namba ya mlipa kodi TIN, Tax Clearance, jina la biashara lililosajiliwa BRELA lenye kuhusisha shughuli za microfinance, finance, credit au microcredit, pamoja na mtaji wa kuanzia wa Shilingi milioni 20.
Kauzeli amesema mwombaji anatakiwa pia kuwasilisha ushahidi wa chanzo cha mtaji huo, picha mbili za passport size, NIDA au cheti cha kuzaliwa, CV pamoja na Credit Reference Report, kabla ya kuwasilisha maombi ya leseni kwa Gavana wa Benki Kuu
Amesema kufanya shughuli za huduma ndogo za fedha bila leseni ni kosa la jinai kwa mujibu wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha Na. 16, hivyo wananchi wanaofanya shughuli hizo wanapaswa kuhakikisha wanapata leseni kabla ya kuanza kutoa huduma.
Kwa upande mwingine, Kauzeli amewataka wananchi kutoa taarifa kwa Benki Kuu endapo watabaini taasisi inayofanya shughuli za huduma ndogo za fedha bila kuwa na leseni, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
Amesema Benki Kuu imeweka orodha ya taasisi zilizopewa leseni kwenye tovuti yake, pamoja na taarifa za Mabenki, taasisi ndogo za fedha, ili wananchi waweze kupata taarifa hizo.
Kwa mujibu wa Kauzeli, hadi Septemba 25, 2026, Benki Kuu ya Tanzania imesajili jumla ya leseni 3,355 za taasisi ndogo za fedha.
Aidha, amewakaribisha wananchi wanaofika kwenye Maonesho ya 9 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita kutembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania ili kupata elimu na maelekezo kuhusu huduma za fedha na masuala mbalimbali yanayosimamiwa na Benki Kuu.

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...