Kamishna wa Polisi Jamii, CP Alex Mkama, amewataka Maafisa Habari wa Jeshi la Polisi kutumia maarifa waliyoyapata katika mafunzo kuboresha utendaji wao na kuendana na mabadiliko ya teknolojia katika tasnia ya habari.

CP Mkama ametoa kauli hiyo wakati akifunga kikao kazi cha Maafisa Habari wa Jeshi la Polisi kilichofanyika katika Chuo cha Polisi Tanzania, Moshi, kuanzia Septemba 28 hadi 30, 2026.

Amesema mafunzo hayo yanapaswa kutafsiriwa kwa vitendo katika maeneo yao ya kazi, akiwataka Maafisa Habari kuwa wabunifu, hususan katika matumizi ya mitandao ya kijamii, ili kufikisha taarifa kwa wananchi kwa haraka, usahihi na kwa wakati.

Aidha, amewataka Maafisa Habari hao kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia nidhamu, haki, weledi, uadilifu na uzalendo, huku wakitambua wajibu wao katika kulinda na kuimarisha amani ya Jeshi la Polisi na nchi kwa ujumla.

CP Mkama pia amewataka kuendelea kuboresha utendaji wao katika tasnia ya habari kwa kutumia maarifa na ujuzi walioupata, akisisitiza umuhimu wa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuhakikisha hawamwangushi Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...