Mkuu wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, Mhe. Edward Mpogolo, amewapongeza walimu wa Kata ya Ukonga kwa kazi kubwa wanayoifanya katika jamii, akisema walimu ni wazalishaji wa wataalamu na viongozi mbalimbali nchini.

Mhe. Mpogolo ameyasema hayo katika sherehe ya walimu wa Kata ya Ukonga inayojulikana kama UKONGA DAY, iliyofanyika Ukonga jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Mpogolo amesema walimu wamekuwa nyenzo muhimu katika jamii kwa kuwaandaa viongozi na wataalamu mbalimbali wanaochangia maendeleo ya Taifa.

Aidha, Mhe. Mpogolo ametoa pongezi hizo kufuatia hotuba ya utangulizi iliyotolewa na mgeni maalum wa hafla hiyo, Mhe. Jerry Silaa, ambaye pamoja na kuwa mlezi wa walimu wa Kata ya Ukonga, pia ana historia ya kipekee na eneo hilo.

Mhe. Silaa amezaliwa katika Kata ya Ukonga na kusoma katika Shule ya Msingi Ukonga. Katika safari yake ya maisha, amekuwa akirejea na kutoa shukrani kwa walimu wa Kata ya Ukonga, akiwatambua kuwa miongoni mwa watu waliochangia mafanikio yake.

Mhe. Mpogolo ameongeza kuwa walimu ni miongoni mwa watu wasiokuwa na wivu katika jamii, kwani wanapowaona watu waliowafundisha wakifanikiwa, hufurahia kuona matunda ya kazi na mchango wao katika kuwaandaa.

Amesema hali hiyo ni tofauti na baadhi ya watu ambao wanapowaona wenzao wakifanikiwa huweza kuwa na wivu, huku walimu wakichukulia mafanikio ya wanafunzi wao kama sehemu ya mafanikio yao wenyewe.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...