Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Aggrey Mwanri, amesema mazungumzo yaliyofanywa na wadau mbalimbali kuhusu hali ya kisiasa nchini yameonesha mwanga mkubwa wa maridhiano na utayari wa wadau hao katika kufikia mwafaka wa pamoja.
Mwanri amesema hayo leo, Septemba 7, 2026, wakati akizungumza katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Kutafakari Hali ya Kisiasa Nchini, uliofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.
Amesema awali, alipowasili kwenye mkutano huo, alikuwa na wasiwasi akidhani kuwa baadhi ya wadau wangekosoa CCM na kukielekezea chama hicho lawama kuhusu changamoto za kisiasa zinazoikabili nchi.
Hata hivyo, amesema mazungumzo yaliyofanyika yameonesha hali tofauti, huku akieleza kuwa utayari wa wadau kushiriki katika majadiliano ya kujenga ni ishara muhimu kuelekea maridhiano na mwafaka.
“Wakati nakuja nilikuwa na hofu kidogo, nikafikiria kwamba watarusha mawe CCM, chama tawala, kwamba hii shida yote tunayopata ni CCM. Tulikuwa na Mzee Wasira, nikamwambia kama mood yenyewe ni hii, unaweza kuwa na uhakika kuwa tuko tayari,” amesema Mwanri.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...