Na Mwandishi wetu,DODOMA

Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeanza awamu ya pili ya kampeni ya chanjo ya polio, ikilenga kuwafikia watoto 250,045 katika kipindi cha siku nne. Zoezi hilo linatarajiwa kukamilika tarehe 2 Oktoba, 2026 huku timu za afya zikielekezwa kuwafikia watoto katika maeneo mbalimbali ya jiji.

Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu wa Huduma za Chanjo Jiji la Dodoma, Victor Kweka aliema "Tumepanga kuwafikia watoto 250,045 katika awamu hii ya kampeni, hivyo tunawaomba wazazi na walezi kushirikiana na wahudumu wa afya ili kuhakikisha watoto wanapata chanjo,” alisema Kweka,

Alisema kuwa maandalizi yamekamilika na juhudi zinaelekezwa kuhakikisha watoto waliolengwa wanafikiwa ndani ya muda uliopangwa.

Kampeni hiyo inalenga kuimarisha kinga dhidi ya polio, ugonjwa wa kuambukiza ambao unaweza kusababisha kupooza na madhara ya kudumu.

Alisisitiza kuwa utoaji wa chanjo unahitaji uelewa na ushiriki wa jamii, huku viongozi wa maeneo wakitakiwa kusaidia katika kuhamasisha wananchi na kufikisha taarifa za kampeni kwa familia.

Kwa kuwa zoezi hilo linafanyika kwa muda mfupi, wazazi na walezi wametakiwa kuchukua hatua mapema badala ya kusubiri siku za mwisho za kampeni. Ushirikiano wao umetajwa kuwa utasaidia timu za afya kuwafikia watoto wengi zaidi na kupunguza uwezekano wa baadhi yao kukosa huduma hiyo muhimu ya kinga.

Kampeni hiyo itahitimishwa tarehe 2 Oktoba, 2026 baada ya siku nne za utekelezaji.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...