Na MWANDISHI WETU
Shri Guru Singh Sabha – Jumuiya ya Sikh Dar es Salaam imekabidhi vifaa 100 vya kuhifadhia taka kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuimarisha usafi na utunzaji wa mazingira jijini.
Akipokea vifaa hivyo , jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, ameishukuru Shri Guru Singh Sabha – Jumuiya ya Sikh Dar es Salaam kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali, hususan maono ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kusimamia usafi na utunzaji wa mazingira.
Mpogolo amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na Jumuiya ya Sikh katika kusaidia huduma mbalimbali za kijamii, kwani mbali na msaada huo, jumuiya hiyo imekuwa ikiandaa kambi mbalimbali za matibabu na vipimo bila malipo.
“Msaada huu ni chachu katika kutekeleza azma ya Rais Dk. Samia ya kulifanya Jiji letu la Dar es Salaam kuwa jiji lenye ushindani katika usafi barani Afrika na kuhakikisha linashika nafasi ya juu,” amesema Mpogolo.
Amesema Serikali wilayani humo itaendelea kusimamia utekelezaji wa azma hiyo na kuzitaka jamii, taasisi, mashirika na wadau mbalimbali kushiriki kikamilifu katika kusimamia usafi na utunzaji wa mazingira.
Awali, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya, amesema mchango huo utaongeza nguvu katika usimamizi wa usafi na mazingira.
“Mwelekeo wa usafishaji wa maeneo yetu hautegemei Halmashauri peke yake. Tunategemeana kati ya Halmashauri na wadau kama Shri Guru Singh Sabha – Jumuiya ya Sikh Dar es Salaam. Tutaendelea kusimamia ushirikiano huu katika kuboresha usafi wa mazingira,” amesema Mabelya.
Shri Guru Singh Sabha – Jumuiya ya Sikh Dar es Salaam pia imeeleza kuthamini ushirikiano mkubwa ambao imekuwa ikiupata kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya.
.Viongozi hao wamekuwa mstari wa mbele kutoa ushirikiano kwa taasisi na jumuiya mbalimbali za kidini, wakitambua kuwa taasisi za dini zina nafasi na wajibu muhimu katika kusaidia kujenga jamii yenye maadili mema, umoja, kuheshimiana, uwajibikaji na mshikamano.
Ushirikiano huo kati ya Serikali na taasisi za kidini unatoa nafasi kwa jumuiya mbalimbali kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na maendeleo, kwa lengo la kujenga jamii bora na yenye maadili kwa manufaa ya wananchi wote.
Mwakilishi wa Shri Guru Singh Sabha – Jumuiya ya Sikh Dar es Salaam, Jasdeep Singh Babhra, amesema mazingira si wajibu wa Serikali pekee bali ni jukumu la jamii nzima, hivyo Jumuiya ya Sikh imeona umuhimu wa kuunga mkono jitihada kubwa za Serikali chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuhimiza utunzaji wa mazingira.
Babhra, amesema Shri Guru Singh Sabha – Jumuiya ya Sikh Dar es Salaam imekabidhi vifaa 100 vya kuhifadhia taka na itaendelea kushirikiana na Serikali katika shughuli mbalimbali za kijamii na maendeleo.
Amesema Jiji la Dar es Salaam linaendelea kukua na kuwa na ongezeko kubwa la watu, hivyo usafi na utunzaji wa mazingira unahitaji ushirikiano wa pamoja kati ya Serikali, taasisi, jumuiya za kidini, sekta binafsi na wananchi.
Diwani wa Kata ya Gerezani, Fatuma Abubakar, amesema Shri Guru Singh Sabha – Jumuiya ya Sikh Dar es Salaam imekuwa mstari wa mbele kushirikiana na Serikali katika kusaidia jamii, hivyo akaishukuru kwa msaada huo wa vifaa muhimu vya usafi.
Shri Guru Singh Sabha – Jumuiya ya Sikh Dar es Salaam imesisitiza kuwa itaendelea kushirikiana na Serikali katika mipango inayolenga kuboresha mazingira, afya, ustawi wa jamii na kujenga jamii yenye maadili, mshikamano na uwajibikaji.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...