Na Vero Ignatus Michuzi Tv Arusha
Tanzania imepiga hatua nyingine katika kujiweka tayari kwa ulinzi na usalama kuelekea Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, baada ya kufungwa kwa mafunzo maalum ya siku tano mkoani Arusha yaliyolenga kuimarisha usalama wa nyuklia na mionzi.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa kushirikiana na Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu (IAEA), yalihusisha vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na taasisi mbalimbali nchini ili kujenga uwezo wa kuzuia, kutambua na kukabiliana na vitisho wakati wa mashindano hayo.
Akifunga mafunzo hayo ya siku tano Jijini Arusha Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya AFCON 2027, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Muliro J. Muliro, alisema kuwa maandalizi hayo ni chachu ya kuhakikisha nchi inakuwa na mifumo madhubuti ya kiusalama.
SACP Muliro aliwataka washiriki kutumia maarifa waliyopata kufanya tathmini katika taasisi zao ili kubaini uwezo uliopo na kufanyia kazi mapungufu mapema, akisisitiza kuwa ukubwa wa mashindano ya AFCON 2027—yatakayoandaliwa kwa pamoja kati ya Tanzania, Kenya na Uganda—unahitaji maandalizi ya kina.
Mafunzo hayo yalichanganya nadharia za darasani na mazoezi ya vitendo, ikiwa ni pamoja na zoezi la kutafuta na kutambua chanzo bandia cha mionzi kilichokuwa kimefichwa. Zoezi hilo lilipima uwezo wa washiriki katika kutumia vifaa, maarifa na taratibu za kiusalama walizofundishwa katika mazingira halisi.
Kwa upande wa sekta ya michezo, Alex Mkenyenge kutoka Idara ya Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, alieleza kuwa usalama wa viwanja na maeneo ya michezo ni nguzo kuu ya maandalizi hayo.
"Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika ujenzi na uboreshaji wa viwanja vya mechi na mazoezi jijini Dar es Salaam, Arusha na Zanzibar. Ni muhimu kuhakikisha miundombinu hii na watu watakaoitumia wanalindwa ipasavyo ili kila anayekuja arejee nyumbani salama," alisema Mkenyenge huku akiishukuru TAEC na IAEA kwa kuongeza utayari wa nchi.
Naye mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Côte d’Ivoire, Lacina Soro, alibainisha kuwa ufanisi wa usalama katika matukio makubwa unategemea ushirikiano kati ya teknolojia na uwezo wa wataalamu, akisisitiza kuwa kuwa na vifaa pekee haitoshi bila uwepo wa mipango madhubuti, tathmini ya vitisho kabla ya tukio, na uratibu mzuri wa mawasiliano kati ya taasisi husika.

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...