MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imeamuru kutolewa kwa wito (summons) kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), ili kutoa ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.

Uamuzi huo umetolewa leo na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dustan Ndunguru baada ya Mahakama kusikiliza hoja za upande wa mashtaka na utetezi kuhusu ombi la Lissu la kuwaita mashahidi hao pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

Mahakama imesema, kwa kuzingatia kifungu cha 314 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), ina hiari ya kuruhusu mashahidi kuitwa kwa kuangalia umuhimu wa ushahidi wao katika shauri.

Katika uamuzi huo, Mahakama imesema imeridhika kuwa ushahidi wa IGP, CDF na DCI ni muhimu katika kesi hiyo, hivyo imeamuru summons zitolewe ili waje kutoa ushahidi upande wa utetezi.

Hata hivyo, Mahakama imekataa ombi la kuwaita baadhi ya mashahidi waliotajwa na Lissu, akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa zamani Kassim Majaliwa, ikisema ushahidi wao hauhusiani na kesi hiyo kwa upande wa utetezi.

Mahakama pia imekubaliana na hoja ya upande wa mashtaka kwamba mashahidi ambao hawakutajwa wakati wa committal proceedings hawawezi kutajwa baadaye wakati wa usikilizwaji wa hoja za awali (PH).

Jaji Ndunguru amesema kifungu cha 281 cha CPA kinaeleza kuwa msajili atatoa summons kwa mashahidi waliotajwa wakati wa committal proceedings, huku Mahakama ikibaini kuwa katika mwenendo wa kesi hiyo hakukuwa na orodha ya mashahidi waliotajwa.

Kuhusu hoja ya kumuita Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Mahakama imesema mfano wa kesi ya Khatibu Ghandi hauwezi kutumika moja kwa moja kwa kuwa katika kesi hiyo shahidi huyo aliitwa na upande wa mashtaka na pia sheria ya sasa ya Usalama wa Taifa haikuwepo wakati huo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho saa tatu asubuhi kwa ajili ya kuendelea na hatua ya utetezi.


Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...