Wadau wa kilimo-misitu nchini Tanzania wameanzisha jukwaa maalum (TASP), litakalowaunganisha wadau mbalimbali kwa ajili ya kubadilishana uzoefu, taarifa na ubunifu, pamoja na kuimarisha ushirikiano katika kuendeleza kilimo-misitu na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.
Akifungua jukwaa hilo Septemba 10, 2026 jijini Dodoma, Afisa Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Nickson Kimaro, amesema kilimo-misitu ni agenda mtambuka inayohitaji ushirikiano wa Serikali, wakulima, taasisi za utafiti, sekta binafsi, asasi za kiraia, taasisi za fedha na washirika wa maendeleo.
Amesema TASP inapaswa kuwa mfumo endelevu wa uratibu utakaowezesha wadau kuoanisha jitihada zao, kubaini mapungufu na kutumia rasilimali kwa ufanisi, huku kilimo-misitu kikiwa na manufaa ya kiuchumi, kijamii na kimazingira.
Mkurugenzi Mtendaji wa Civic Social Protection Foundation (CPS), Nemence Iriya, amesema jukwaa hilo litatoa nafasi kwa wadau kukutana na kujadili sera, mikakati, sheria na taratibu zinazohusu kilimo-misitu, pamoja na kuimarisha uratibu wa shughuli zao.
Amesema TASP pia itasaidia kuhakikisha matokeo ya tafiti na ubunifu unaofanywa na watafiti unawafikia wakulima moja kwa moja, pamoja na watunga sera na wafanya maamuzi, na kuhalikisha tafiti hizo zinatumika katika kuboresha mipango na mikakati ya kilimo-misitu.
Kwa upande wake, Afisa Utafutaji Rasilimali Fedha, Mawasiliano na Utetezi kutoka VI-Agroforestry, Khalid Ngassa, amesema jukwaa hilo litawawezesha wadau kukutana pamoja, kubadilishana maarifa na uzoefu na kujadili changamoto zinazowakabili ili kupata suluhisho kwa pamoja.
Kwa ujumla, kuanzishwa kwa jukwaa hilo, kunatoa fursa muhimu ya kuwaunganisha wadau wa kilimo-misitu na kujenga mshikamano katika kushughulikia changamoto zinazowakabili, huku mafanikio ya jukwaa hilo yakitegemea utekelezaji wa mijadala na maazimio yaliyowekwa ili kuleta matokeo yanayoonekana kwa wakulima, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na maendeleo ya sekta hiyo nchini.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...