Na Jane Mwakyoma.
MKUU wa Mkoa wa Rukwa Charles Makongoro amewaongoza viongozi na wananchi wa Manispaa ya Sumbawanga kufanya zoezi la usafi katika Soko Kuu la Manispaa hiyo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi na tahadhari dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa.
Zoezi hilo lilihusisha usafishaji wa maeneo mbalimbali ya soko na kuzibua mifereji ya maji ili kupunguza uwezekano wa mafuriko.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo Makongoro amewataka wananchi kuendeleza usafi katika maeneo yao ya makazi na biashara, akisisitiza kuwa usafi wa mazingira unapaswa kuwa utamaduni wa kila siku na si kufanyika wakati wa zoezi maalumu pekee.
“Maandalizi ya mapema ni muhimu. Kila mmoja wetu anapaswa kuhakikisha eneo analoishi au kufanyia biashara ni safi na mifereji ya maji haijazibwa,” amesema.
Tahadhari hiyo inaendana na utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wa Agosti 18, 2026, kuhusu msimu wa Vuli wa Oktoba hadi Desemba 2026, ambapo TMA ilieleza kuwa msimu huo unatarajiwa kuathiriwa kwa kiwango kikubwa na hali ya El NiƱo katika Bahari ya Pasifiki huku mvua za Vuli zikitarajiwa kuwa za juu ya wastani hadi wastani katika maeneo mbalimbali nchini.
Baadhi ya wananchi walioshiriki zoezi hilo wamepongeza viongozi kushiriki moja kwa moja katika usafi, wakisema hatua hiyo inaweza kuongeza hamasa kwa jamii kuchukua tahadhari mapema na kuwa usafi wa mazingira si jukumu la Serikali pekee bali wafanyabiashara, familia, taasisi na makundi mbalimbali ya jamii wanapaswa kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi na mifereji inazibuliwa
Pia wameomba elimu kuhusu El Nino na athari za mvua kubwa itolewe kwa wakati na kwa lugha rahisi ili wananchi waweze kuelewa ni athari gani zinapaswa kuchukuliwa.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...