IRINGA: Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa,
Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndugu Rabia Abdalla Hamid, ametembelea na kukagua miradi ya wanufaika wa mikopo inayotolewa na Halmashauri kwa makundi maalum mkoani Iringa.
Rabia amefanya ziara hiyo leo, Septemba 21, 2026, wakati wa ziara yake ya kusikiliza makundi mbalimbali ya kijamii mkoani humo.
Akizungumza baada ya kutembelea na kukagua miradi hiyo, Rabia amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kuhakikisha wanarejesha kwa wakati ili fedha hizo ziendelee kunufaisha makundi mengine yenye uhitaji.
Amesema Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa makundi yote yanayostahili kupata mikopo hiyo ili kuwawezesha kiuchumi na kuongeza fursa za kujiajiri.
Aidha, Rabia amezitaka Halmashauri kuendelea kuongeza kasi katika utoaji wa mikopo kwa makundi yenye sifa, huku akisisitiza umuhimu wa fedha hizo kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta tija kwa wanufaika.
Amesema utekelezaji mzuri wa programu hiyo unahitaji ushirikiano kati ya Halmashauri na wanufaika, hususan katika kuhakikisha mikopo inarejeshwa kwa wakati na inawafikia wananchi wengine.




.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...