Vodacom Tanzania PLC, kwa kushirikiana na Oakwood Holdings Limited, imehitimisha mashindano ya Vodacom Corporate Masters 2026 yaliyofanyika katika Uwanja wa TPDF Lugalo Golf Club, yakiwakutanisha wachezaji wapatao 150 kutoka Tanzania na nchi jirani, wakiwemo viongozi wa biashara, wakurugenzi na wakuu wa makampuni pamoja na wapenzi wa mchezo wa golf.
Wachezaji gofu Khalid Shemndolwa na Yvonne Ondari wameibuka washinda kwa jumla shindano la Vodacom Corporate Masters kwa upande wa wanaume na wanawake. Katika shindano hilo lililofanyika kwenye uwanja wa Lugalo, Shemndolwa alikusanya pointi 42 huku Ondari akikusanya pointi kama hizo katika mashindano hayo ya siku moja.
Mbali ya Shemndolwa na Ondari, Godfrey Abel aliibuka mhsindi katika daraja A, kwa kupata pointi 42, akifuatiwa na Likuli Juma aliyepata pointi 41 ambapo Sigfrid Urassa alitwaa ubingwa wa daraja B kwa pointi 40, akimzidi Godfrey Kilenga aliyemaliza na pointi hizo hizo, lakini Urassa akashinda kwa kanuni ya countback.
Boniface Japhet alitwaa ubingwa wa daraha C baada ya kupata pointi 39, huku Abdallah Singano akimaliza nafasi ya pili kwa pointi 37. Kwa upande wa wanawake, Neema Job alimaliza na pointi 42 na kutwaa ubingwa, akifuatiwa na Leticia Kapalia aliyepata pointi 40. Mashindano ya timu za kampuni nayo yalikuwa kivutio kikubwa, huku timu ya KQ ikiibuka mshindi baada ya kushindana na timu nyingine tisa za kampuni.
Zawadi maalum za mtu mmoja mmoja zilienda kwa Michael Norbert aliyeshinda Longest Drive kwa wanaume, huku Kapalia akitwaa tuzo hiyo kwa wanawake. Harshid Barmeda alishinda Nearest to the Pin kwa wanaume, wakati Vaileth James akitwaa tuzo hiyo kwa wanawake.
Mbali na ushindani, washiriki pamoja na familia zao walifurahia shughuli mbalimbali katika eneo la Corporate Village, lililokuwa na burudani, maonesho ya biashara, magari ya zamani pamoja na eneo maalum la watoto.
Mkurugenzi wa Vodacom Business wa Vodacom Tanzania PLC, Nguvu Kamando, alisema mashindano hayo yameendelea kuonyesha nafasi ya michezo katika kujenga mahusiano yenye tija katika biashara.
“Vodacom Corporate Masters 2026 Golf Cup imethibitisha tena kwamba michezo ni jukwaa lenye nguvu katika kujenga mahusiano ya muda mrefu ya kibiashara. Tunafurahishwa na ushiriki mkubwa wa kampuni na kasi ya mahusiano mapya yaliyojengwa wiki hii,” alisema Kamando.
Mwenyekiti wa Kamati ya Corporate Masters, Ken Kariuki, alizipongeza kampuni zilizoshiriki na kusema mashindano hayo yanaendelea kuchangia katika kujenga mtandao wa kibiashara na kukuza mchezo wa gofu.
“Mwaka huu tulishuhudia ushindani wa kiwango cha juu uwanjani na ushiriki wenye maana katika biashara nje ya uwanja. Hilo ndilo lengo kuu la Corporate Masters, kuzikutanisha kampuni katika mazingira rafiki yanayozalisha fursa halisi za ushirikiano,” alisema Kariuki.
Alisema ushirikiano kati ya Vodacom na Corporate Masters unaonyesha namna kampuni zinavyoweza kufanya kazi pamoja katika kutengeneza thamani kwa wateja na wadau, huku zikiunga mkono maendeleo ya mchezo wa gofu nchini Tanzania.
Kufanikiwa kwa mashindano ya Vodacom Corporate Masters 2026 kunaendelea kuthibitisha mkakati wa Vodacom Tanzania wa kutumia michezo kama jukwaa la kuimarisha mahusiano ya kibiashara, kuhamasisha ubunifu na kuwasogeza karibu viongozi wa biashara na suluhisho za kidijitali zinazochochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania.
Mshindi wa jumla kwa upande wa wanawake, Yvonne Ondari (wa tatu kushoto), akipokea zawadi baada ya kutwaa taji katika Vodacom Corporate Masters 2026 Golf Tournament yaliyofanyika Lugalo Golf Club mwishoni mwa wiki. Ondari alikusanya pointi 42 (CB) katika mashindano yaliyoshirikisha wachezaji golf 150 kutoka Tanzania na nje ya nchi.
Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando (kushoto), akikabidhi zawadi ya tiketi ya kwenda na kurudi Mauritius kwa mshindi wa jumla kwa wanaume Khalid Shemndolwa (wa tatu kushoto) katika mashindano ya Vodacom Corporate Masters 2026 Golf Tournament yaliyofanyika Lugalo Golf Club, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Shemndolwa alikusanya point 42 katika mashindano yaliyoshirikisha wachezaji gofu 150 kutoka Tanzania na nje ya nchi.
Washindi wa Vodacom Corporate Masters 2026 Golf Tournament katika makundi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupokea zawadi zao, Tukio hilo lilifanyika Lugalo Golf Club, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
.jpeg)
Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando, akishiriki mashindano ya Vodacom Corporate Masters 2026 Golf Cup yaliyofanyika Lugalo Golf Club, Dar es Salaam, Septemba 5, 2026. Mashindano hayo yalishirikisha wachezaji gofu 150 kutoka Tanzania na nje ya nchi.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Uwezeshaji wa Vodacom Business Joseph Sayi, akishiriki mashindano ya Vodacom Corporate Masters 2026 Golf Cup yaliyofanyika Lugalo Golf Club, Dar es Salaam, Septemba 5, 2026. Mashindano hayo yalishirikisha wachezaji gofu 150 kutoka Tanzania na nje ya nchi.

Washindi wa Vodacom Corporate Masters 2026 Golf Tournament katika makundi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupokea zawadi zao, Tukio hilo lilifanyika Lugalo Golf Club, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.jpeg)
Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando, akishiriki mashindano ya Vodacom Corporate Masters 2026 Golf Cup yaliyofanyika Lugalo Golf Club, Dar es Salaam, Septemba 5, 2026. Mashindano hayo yalishirikisha wachezaji gofu 150 kutoka Tanzania na nje ya nchi.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Uwezeshaji wa Vodacom Business Joseph Sayi, akishiriki mashindano ya Vodacom Corporate Masters 2026 Golf Cup yaliyofanyika Lugalo Golf Club, Dar es Salaam, Septemba 5, 2026. Mashindano hayo yalishirikisha wachezaji gofu 150 kutoka Tanzania na nje ya nchi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...