Jumla ya watoto wachanga 15 wenye changamoto ya manjano na watoto zaidi ya 30 njiti hupokelewa kila mwezi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita. Changamoto hizo zimekuwa zikisababisha vifo vingi kwa watoto wachanga.

Hali hiyo imeiibua Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Geita kuona ipo haja ya kuongeza nguvu katika mapambano ya kuwaokoa watoto hao.

TAKUKURU Mkoa wa Geita imetoa vifaa vya kuokoa watoto njiti na wenye manjano, ambavyo ni infant warmer pamoja na photo therapy kwa ajili ya kuzuia vifo vya watoto wachanga.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Nchini, Neema Mwakalyele amesema zoezi la kukabidhi mashine hizo katika hospitali mbalimbali limefanyika katika zaidi ya mikoa 20 nchini.

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita imepatiwa jumla ya mashine 6 za aina hiyo, wakati mahitaji ni jumla ya mashine 10 ili kumaliza kabisa vifo vya watoto njiti na wenye manjano.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mheshimiwa Alexander Pastory Mnyeti, ameishukuru TAKUKURU kwa vifaa hivyo ambavyo vinaenda kuokoa maisha ya watoto wachanga. Amesema atahakikisha anachangia kupatikana kwa mashine zilizobaki ili kumaliza kabisa changamoto hiyo.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...