Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Ndg. Abdi Mahmoud Abdi, amesema uwepo wa maskani za vijana wa CCM ni miongoni mwa njia muhimu za kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa wanachama na viongozi wa chama katika ngazi mbalimbali.
Ndg. Abdi ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Maskani ya CCM ya Kibweni Shaba Juu, iliyopo katika Jimbo la Mkwajuni, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema maskani zina nafasi muhimu katika kuwakutanisha wanachama, hususan vijana, na kuwawezesha kubadilishana mawazo, kujenga na kuimarisha mahusiano, pamoja na kushirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo na za chama.
Aidha, Ndg. Abdi amewataka wana-CCM na wanamaskani kuendelea kudumisha umoja na mshikamano uliopo nchini, sambamba na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na viongozi wakuu wa nchi na chama katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Amesisitiza kuwa umoja, mshikamano na ushirikiano ni msingi muhimu katika kuendelea kuijenga CCM imara, yenye uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kwa manufaa ya wananchi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...