Na Janeth Raphael - MichuziTv
Migogoro ya ardhi imeendelea kuwa miongoni mwa changamoto kubwa zinazowasilishwa na wananchi kupitia kipindi cha Sema na Waziri, hali ambayo imeifanya Serikali kuendelea kutathmini upya mfumo wa utatuzi wa migogoro hiyo ili kupata njia yenye ufanisi zaidi.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Homera, amesema asilimia kubwa ya malalamiko yanayowasilishwa katika kipindi hicho yanahusu migogoro ya ardhi, akieleza kuwa Serikali inaendelea na uchambuzi wa kina wa sheria inayosimamia mabaraza ya ardhi nchini.
Dkt. Homera amesema uchambuzi huo unalenga kubaini iwapo mabaraza hayo yanapaswa kuongezewa nguvu na mamlaka ili yaweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi, au endapo majukumu hayo yanaweza kuhamishiwa katika mfumo wa mahakama.
Amesema kwa sasa mabaraza ya ardhi yamebaki zaidi katika jukumu la usuluhishi, hivyo Serikali inataka kutathmini namna bora ya kuimarisha utendaji wake ili yaweze kuwa na mchango mkubwa zaidi katika kutatua migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi.
Kwa mujibu wa Dkt. Homera, hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha wananchi wanapata ufumbuzi wa changamoto zao kwa wakati, hususan migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikichukua muda mrefu na kuathiri maisha na shughuli za wananchi.
Amesema hatua hiyo pia inatekelezwa kufuatia maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha changamoto zinazowakabili wananchi zinapatiwa ufumbuzi na mifumo ya utoaji haki inaendelea kuimarishwa.
Dkt. Homera ameyasema hayo leo Septemba 25, 2026, jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kipindi cha Sema na Waziri, ambapo ameeleza hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuboresha mifumo ya haki na sheria nchini.
Waziri huyo amejiwekea utaratibu huo wa kuzungumza na wananchi Moja kwa moja ( KUpitia simu) ili wananchi waeleze changamoto za kisheria zinazowakabili.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...