Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe, ameiagiza Bohari ya Dawa (MSD) kuharakisha mchakato wa upatikanaji na usambazaji wa dawa ya kutibu uraibu wa pombe ‘Naltrexone’ kwa ajili ya Taasisi ya Afya ya Akili Tanzania (TMHI), na kuhakikisha upatikanaji wake unakuwa endelevu.
Dkt. Magembe amesema hayo wakati wa mafunzo maalum yaliyoandaliwa na TMHI kuhusu matumizi sahihi ya ‘Naltrexone’ katika usimamizi wa tiba uraibu wa pombe yanayofanyika kwa siku tatu Jijini Dodoma, kuanzia Septemba 2, 2026.
“Watu wameshasikia MSD inaleta dawa hii, sasa ni vyema tukajua dawa hii inaanza kupatikana lini?” amehoji Dkt. Magembe, huku akiiagiza MSD kuhakikisha dawa hiyo inapatikana ifikapo mwisho wa mwezi Septemba 2026, ili wataalamu wanaopatiwa mafunzo waweze kuielewa kwa ajili ya matumizi watakapoanza kutoa kuitumia huduma hiyo.
Dkt. Magembe amesema unywaji wa pombe kupindukia umekuwa miongoni mwa changamoto zinazoweza kuathiri afya ya akili, ustawi wa jamii, kuchangia mmomonyoko wa maadili, vitendo vya ukatili, migogoro kwenye familia pamoja na ajali za vyombo vya moto, hivyo ni wakati sasa wa kupunguza matatizo haya.
Akitoa ufafanuzi kuhusu upatikanaji wa dawa hiyo ya Naltrexone, Msimamizi wa Dawati la Wateja wakubwa wa MSD, Mfamasia Michael Bajile, amesema MSD tayari imekamilisha mchakato wa zabuni ya ununuzi wa bidhaa hiyo na watahakikisha inawasili nchini kwa wakati na kuendelea kupatikana kadri ya mahitaji ya TMHI.
“Ni matarajio yetu kwamba baada ya mafunzo haya kwa wataalamu wetu wa afya, ndani ya mwezi huu Septemba bidhaa hii itakuwa imeingia nchini na usambazaji utafanyika mara moja katika Taasisi ya Afya ya Akili Tanzania,” amesema Bajile.
Mafunzo hayo yanalenga kuwaongezea wadau wa TMHI uelewa na uwezo wa kutumia Naltrexone kwa usahihi na usalama, pamoja na kuimarisha utoaji wa huduma za matibabu kwa watu wenye changamoto ya Alcohol Use Disorder kwa kuzingatia ushahidi wa kisayansi.



.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...