Na Victor Masangu,Kibaha 

Katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya elimu Mstahiki Meya wa Halmashauri ya  Manispaa ya Kibaha ameahidi kuimarisha mazuri ya ufundisha  kwa kujenga ofisi ya walimu katika shule ya Msingi Zegereni.

Hayo ameyabainisha  wakati wa mahafali ya pili ya Shule ya Msingi Zegereni iliyopo Kata ya Visiga, iliyopo katika  Manispaa ya Kibaha na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wakiwemo wazazi pamoja na walezi

Amebainisha kwamba lengo lake kubwa ni kuweka mikakati madhubuti ya kuwasaidia walimu wawe na mazingira mazuri ya ufundishaji na kuondokana na changamoto ya kutokuwa na ofisi.

"Hawa watoto wetu ni tunu ya Taifa kwa hivyo wanapaswa kupatiwa misingi mizuri ya elimu ndio maana katiks hili nitahakikisha walimu wetu wanakuwa na ofisi nzuri ambazo zitawasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuboresha elimu,'alisema Mstshiki Meya.

Pia Dkt Nicas amesema, wanafunzi wanatakiwa kuwa wazalendo  pamoja na kusoma kwa bidii ili kufikia malengo yaliyowekwa na serikali ya elimu ya lazima kuwa ni  kidato cha nne. 

"serikali ya Dkt Samia imelenga katika kuona miundo mbinu ya  elimu inaboreshwa zaidi na kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwenye mazingira mazuri na wanapata elimu inayostahili", amesema Dkt Nicas.

Amesema, kila  mwanafunzi anawajibika kwa nafasi yake ili aweze kufanya vizuri kwenye masomo yao kwa sababu taifa linawategemea. 

Dkt Nicas ameendelea kusisitiza wazazi wasiwaachie walimu majukumu yote kwa sababu wao pia wanatakiwa kushiriki katika masuala yote hanayohusu elimu ikiwemo kuchangia baadhi ya michango midogo midogo ya uendeshaji wa shule.

Naye mmoja wa wanafunzi ambaye amehitimu darasa la saba katika shule hiyo ya Zegereni akisoma risala kwa niaba ya wenzake ameiomba serikali kuwasaidia kupata uzio katika shule hiyo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...