Na Mwandishi wetu, Simanjiro 

MDAU wa maendeleo wa Mkoa wa Manyara, Taiko Kulunju Ole Tipa ameongoza harambee na kupatikana shilingi milioni 17 laki mbili na Elfu 27 na dume moja la ng'ombe ili kuwawezesha kiuchumi wanawake wa jamii ya wafugaji kikundi cha Enyoroto kijiji cha Kimotorok Kata ya Loiborsiret, Wilayani Simanjiro.

Taiko akizungumza kwenye harambee hiyo amesema wanawake hao wa kikundi cha Enyoroto wanapaswa kuwezeshwa kwani wana mchango mkubwa kwa jamii na ukimuwezesha mwanamke umeiwezesha jamii.

"Mama zetu wa jamii ya kifugaji wamebadili maisha yao kiuchumi na familia za hivyo tunawawezesha pia kuunga mkono jitihada za Rais wetu mpendwa Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii," amesema Taiko.

Amesema wanawake wa Simanjiro wamekuwa wakipambana kuichumi kwa maslahi mapana ya wao wenyewe, familia zao, jamii na Taifa kwa ujumla hivyo wanapaswa kuungwa mkono.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kikotorok, Elias Parmelo, ametoa shukrani za dhati kwa mdau wa maendeleo Taiko kwa jitihada na moyo wake wa kujitolea katika kusaidia shughuli mbalimbali za maendeleo zinazolenga kuboresha maisha ya watu

Parmelo amepongeza namna Taiko Kulunju anavyoendelea kushirikiana na jamii kwa vitendo, akieleza kuwa mchango wake ni mfano wa uzalendo, mshikamano na kujali maendeleo ya wananchi.

“Tunamshukuru sana Taiko Kulunju kwa moyo wake wa kusaidia jamii, tunathamini kazi anayofanya na tunaomba Mungu aendelee kumpa nguvu, afya na uwezo wa kuendelea kuwa sehemu ya maendeleo ya Kimotorok na jamii kwa ujumla,” amesema Parmelo. 

Katibu wa UWT Wilaya ya Simanjiro, Tichomo in Sangija amesema kutokana na mchango huo mkubwa wa Taiko, wanawake wa jamii ya kifugaji wa Kimotorok wameanza kubadili maisha yao kiuchumi kwa kupata fursa za uwezeshaji.

"Hatua hii ya uwezeshaji inasaidia kuongeza kipato na kujenga uwezo wa kujitegemea katika familia zao kwani kwa muda mrefu, wanawake katika jamii za wafugaji wamekuwa wapambanaji," amesema Sangija.

Mmoja kati ya wanufaika wa Enyoroto Esupat Solomon amesema wamekuwa wakishiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji, ikiwemo ufugaji, biashara ndogo ndogo ila changamoto za ukosefu wa mtaji zimekuwa kikwazo hivyo uwezeshaji wa Taiko utawasaidia zaidi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...