Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Geita, Manjale Magambo, ametembelea kiwanda kikubwa cha kutengeneza mabasi cha Yutong kilichopo Zhengzhou nchini China kwa mwaliko rasmi.

Ziara hiyo inalenga kujifunza teknolojia na mbinu za kisasa zinazotumika katika sekta ya usafirishaji ili kuona namna zinavyoweza kusaidia kukuza uchumi na kufungua fursa kwa vijana nchini.

Akiwa kiwandani hapo, Magambo alipata fursa ya kujionea kwa vitendo mchakato mzima wa uzalishaji wa mabasi, kuanzia usanifu hadi hatua za mwisho, jambo lililompa uelewa wa karibu kuhusu teknolojia na mifumo bora inayotumika

Akizungumza baada ya ziara hiyo, Magambo alisema China imefanikiwa kuitumia sekta ya usafirishaji kama injini muhimu ya maendeleo ya uchumi kwa kuunganisha teknolojia na ufanisi.

 “Ziara hii imetupa nafasi ya kujifunza na kuona kwa vitendo namna teknolojia inavyotumika katika sekta ya usafirishaji. Tumepata uzoefu ambao tunaweza kuutumia katika kutafakari fursa mbalimbali za maendeleo na kuwawezesha vijana kushiriki zaidi katika uchumi,” alisema Magambo.

Aliongeza kuwa uzoefu aliopata ni muhimu kwa vijana wa Kitanzania kufahamu fursa zilizopo katika sekta ya usafirishaji, zikiwemo uwekezaji, ajira na ujasiriamali.

Kwa mujibu wake, vijana wanapaswa kuwa tayari kujifunza teknolojia na mifumo mipya ya uzalishaji kutoka sehemu mbalimbali duniani kwani dunia inabadilika kwa kasi na teknolojia imekuwa nguzo ya maendeleo.

Magambo alisisitiza kuwa maarifa hayo hayapaswi kuishia kwenye ziara pekee, bali yanapaswa kutumika kujenga mawazo mapya yatakayosaidia kuongeza ajira na shughuli za kiuchumi kwa vijana na wananchi kwa ujumla.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...