Wafanyabiashara wa Kariakoo wanatarajiwa kupata fursa zaidi za mauzo na kupokea malipo kwa njia za kidijitali kupitia Kariakoo Festival 2026. Benki ya NMB imetangaza udhamini wa Sh milioni 165 kwa tamasha hilo litakalofanyika Septemba 25 hadi 27 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Msimu wa tatu wa tamasha hilo ulizinduliwa Septemba 8 kwa msafara maalumu uliopita katika barabara na mitaa mbalimbali ya Kariakoo kabla ya kuishia Soko Kuu la Kariakoo. Uzinduzi uliongozwa na Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, Ashraph Abdulkarim, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo.

Mkuu wa Idara ya Biashara wa NMB, Alex Mgeni, alisema wafanyabiashara watapata huduma za kupokea malipo kupitia NMB Lipa Namba na NMB Mkononi. Watapata pia nafasi ya kutumia NMB Tap pamoja na taarifa kuhusu Mshiko Fasta na NMB SME World Business Credit Card kwa ajili ya mahitaji ya mitaji.

Abdulkarim alisema tamasha hilo litawasaidia wafanyabiashara kuuza bidhaa kwa bei za punguzo na kupunguza mizigo iliyopo maghalani kuelekea mwisho wa mwaka. Waandaaji wamewahimiza wafanyabiashara kujisajili mapema na wanunuzi kujitokeza kwa wingi.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...