Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imetunukiwa tuzo maalum katika Jukwaa la Fungua fursa mkoa wa Geita, ikiwa ni kutambua mchango wa Ofisi katika utoaji wa huduma za Elimu na Ushauri wa Kisheria nchini na kwa wananchi na Washiriki wa Maonesho ya Kitaifa ya Madini yanayofanyika Mkoani Geita.
Tuzo hiyo imetolewa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Septemba 25, 2026, na kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Hashim Abdallah Komba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Alexander Mnyeti, Tuzo hiyo imepokelewa na Wakili wa Serikali Mkoa wa Kagera Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Richard Nkaina.
Aidha, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inashiriki katika Jukwaa la Fungua Fursa mkoa wa Geita kwa Kutoa elimu na Ushauri wa Kisheria kwa Wananchi wa Mkoa huo.
Uzinduzi rasmi wa Jukwaa la Fungua Fursa unafuatiwa na Maonesho ya Kitaifa ya Madini yalioanza tarehe 23 Septemba, 2026 na yataendelea hadi tarehe 3 Oktoba 2026 katika Viwanja vya Maonesho vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, mjini Geita.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...