Na Janeth Raphael - MichuziTv Bungeni -Dodoma
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema Serikali zote mbili zimekubaliana kuondoa suala la mafuta na gesi asilia kwenye Orodha ya Masuala ya Muungano.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Reuben Kwagilwa, wakati akijibu swali la Mbunge Rashid Habib Ali Rashid (Mtambwe), aliyetaka kujua kama Serikali ina mpango wa kuondoa suala la mafuta na gesi kwenye Orodha ya Masuala ya Muungano.
Akijibu swali hilo, Kwagilwa amesema Serikali zote mbili zimekubaliana kuondoa Jambo la 15, linalohusu maliasili ya mafuta, mafuta yasiyochujwa ya motokaa, petroli na aina nyingine za mafuta au bidhaa pamoja na gesi asilia, kwenye orodha hiyo.
Amesema hatua hiyo inakwenda sambamba na hali ya sasa ambapo suala la mafuta na gesi asilia tayari linasimamiwa na kila upande wa Muungano kupitia sheria na mamlaka zake.
Kwa upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Naibu Waziri amesema imetunga Sheria ya Mafuta na Gesi Asilia ya Mwaka 2015, ambayo chini ya Kifungu cha 11 ilianzisha Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kwa ajili ya kusimamia shughuli za sekta hiyo.
Kwa upande wa Zanzibar, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetunga Sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Namba 6 ya Mwaka 2016, iliyoanzisha Mamlaka ya Udhibiti, Utafutaji na Uendelezaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar (ZPRA).
Aidha, sheria hiyo imewezesha kuanzishwa kwa Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar (ZPDC).
Kwa mantiki hiyo, Serikali imeeleza kuwa hatua ya kuondoa mafuta na gesi asilia kwenye Orodha ya Masuala ya Muungano inaendana na mfumo ambao tayari umewekwa wa kila upande kusimamia shughuli za sekta hiyo kwa mujibu wa sheria na taasisi zake.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...