
LIGI Kuu ya Hispania (LaLiga) itaendelea na msisimko wake leo, Septemba 11, ambapo Sevilla watawakaribisha Valencia katika uwanja wao wa nyumbani, Estadio Ramón Sánchez Pizjuán, jijini Seville. Mechi hii ya mzunguko wa tano itaanza saa 22:00 usiku,
Sevilla, chini ya uongozi wa kocha Luis García, wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa nafasi ya saba kwenye msimamo wakiwa na pointi saba kutoka mechi nne. Timu hiyo ilianza vizuri kwa ushindi wa nyumbani wa 2-1 dhidi ya Rayo Vallecano, ikafuatiwa na ushindi wa 3-1 ugenini dhidi ya Athletic Club, kabla hali kuanza kubadilika. Baadaye walifungwa 3-1 nyumbani dhidi ya Atletico Madrid, na wikendi iliyopita walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Espanyol huko nje.
Jambo la kushangaza ni kwamba Sevilla walicheza sehemu kubwa ya mchezo huo dhidi ya Espanyol wakiwa na wachezaji kumi tu, na licha ya kuongoza mapema nusu ya pili, walifungwa goli dakika ya 98 na kupoteza ushindi uliokuwa mikononi mwao.
Upande wa pili, hali ni tete zaidi kwa Valencia. Timu ya kocha Carlos Corberán inashika mkia wa msimamo (nafasi ya 20) ikiwa na pointi moja tu kutoka mechi nne, jambo linaloashiria msimu mgumu tangu mwanzo. Katika mchezo wao wa mwisho, Valencia walipigwa vibaya 5-0 nyumbani dhidi ya Barcelona.
Kocha Corberán mwenyewe alikiri hali hiyo baada ya mechi, akisema kwamba dhidi ya timu kubwa kama Barcelona, kila kitu lazima kiende sawasawa ili kupata matokeo mazuri, jambo ambalo halikutokea kwao siku hiyo.
Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Kwa sasa Valencia wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa hawajapata ushindi kwa mfululizo wa michezo kadhaa, huku baadhi ya ripoti zikieleza kuwa wana changamoto kubwa ya majeruhi kambini kwao, jambo litakalomfanya Corberán ajitahidi zaidi kupanga kikosi chake ili apate ushindi wa kwanza.
Valencia hawajafungwa katika michezo sita ya mwisho dhidi ya Sevilla, na wameshinda mechi mbili kati ya tatu za mwisho walizokuja uwanjani hapa. Katika mchezo wao wa mwisho msimu uliopita, Valencia walishinda 2-0 ushindi uliothibitisha uwezo wao wa kuizuia Sevilla licha ya kutokuwa na fomu nzuri wakati huo.
Kwa ujumla, hii ni mechi ya "lazima kushinda" kwa pande zote mbili kwa sababu tofauti Sevilla wanataka kurejea kwenye ushindi baada ya wiki mbili za kutofunga, huku Valencia wakitafuta ushindi wao wa kwanza wa msimu ili kutoka chini kabisa ya msimamo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...